
Kutengeneza mpangilio katika taaluma yangu.
Kama ninapenda
ninachofanya, ninarahisisha mambo mengi, nitabadilisha namna
ninavyofanya kazi na kutafuta watu sahihi ili niweze kufanya kazi ambayo
mimi peke yangu siwezi. Hili jambo linawezekana kama unapenda
unachofanya.
Katika Ufanisi na Utendaji.
Kwasababu
unapenda unachofanya hata ufanisi unaongezeka. Wakati wote unatafuta
namna ya kuboresha unachokifanya, kwasababu hufanyi kwa ajili ya watu
wengine bali kwaajili yako mwenyewe, na hilo huleta matokeo tofauti na
bora zaidi.
Mahusiano yako na watu yanakuwa bora zaidi
Tunasikia kuhusu
siasa, kazi zinapokuwa nyingi ofisini, mabosi kunyanyasa wafanyakazi
wao n.k. Mambo hayo huwa mara nyingi yanakuwa rahisi kwa mtu anayependa
anachokifanya, vitu vingi unakuwa unafanya bila kusukumwa na mtu.
Inamaanisha unakuwa na uhusiano wako mzuri na bosi wako kwani kazi yako
inafanyika kwa wakati na ubora sahihi kwa sababu unapend na kile
unachokifanya.
Kwa kawaida
ninamaanisha kutoacha nafasi ya kile tunachokipenda na kupenda kile
tunachokifanya.Kama tunataka kuwa na furaha na kufurahia kile
tunachokifanya itatufanya kuwa watu bora zaidi kwenye maisha binafsi na
hata maisha ya kitaaluma.
Inaonekana kana
kwamba haiwezekani, lakini inawezekana. Uwezo wako wa kupenda kufanya
kitu unatakiwa uwe zaidi ya vikwazo unavyokutana navyo ofisini au kwenye
biashara. Hivyo chagua kazi unayoipenda na hautakuja kufanya kazi tena
maishani mwako, kwani kazi yako itakuwa ni maisha yako na si kazi kama
kazi.
إرسال تعليق