Taarifa waliyoitoa inaanza kwa kusema >>
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo
wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa
kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea
ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki
katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu
yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya
kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo
dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom
kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa
mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za
kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu
nchini tumezishuhudiaChangamoto hizo ikiwemo upangaji wa ratiba usiokuwa
na uwiano mzuri.
Baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo, wizi wa
mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,
uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira
katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka
propaganda chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa
ligi ndogo kama ya Tanzania.
Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1. Klabu imehaidiwa kununuliwa na inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta
na kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo
kutumiwa na timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo
ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma.
Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 hii
ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya
ndani kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji
wa basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika
gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo
na wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa
zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la
wachezaji taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda
mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu.
2. Propaganda kuwa Mwalimu Juma Mwambusi
kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi ili apange kikosi dhaifu siku ya
mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha) Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la
Mbeya,kwa maana hiyo ni mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na
timu yetu kwa muda mrefu sasa na ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno
yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka mzunguko wa pili wa ligi kuanza.
maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo wa timu ili ianze
kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha mwalimu
wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu amefedheheshwa sana na taarifa hizo.
3. Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji ndiyo wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka
huu ndani na nje ya uwanja muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka
nini.Mpira ndiyo ajira yao kama watumishi wa umma ndani ya Halmashauri
ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo
la kupanga matokeo.
Klabu yetu haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira
wa miguu kwani tunajua fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama
taifa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na
kutoka sare. Klabu inaamini kuwa timu iliyojiandaa vizuri kama yetu
inastahili kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya timu yetu
ni kushinda mechi kwa kucheza mpira unaovutia na kuwaburudisha
watazamaji.
Tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza
kuota mizizi hasa ligi inapoingia mzunguko wa pili ,katika suala hili
kama ambavyo linataka kuhusishwa nasi yawezekana propaganda hizi kwa
upande wa timu inayotuhumiwa kuandaa michakato hiyo wana uzoefu nalo na
yumkini ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia hatua hiyo
waliofikia sasa.
Kama timu hiyo inauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo
wote iweje ishindwe kuwa na timu imara na ya ushindaji mpaka itegemee
kutafuta wachezaji wa timu pinzani kupata matokeo mazuri?
Timu yetu ndiyo timu pekee changa miongoni mwa timu tano
zinazoongoza msimamo wa ligi yetu kwa sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu
pekee inayoundwa na wachezaji wengi wapya katika ulimwegu wa soka na
inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia wachezaji,benchi la ufundi
pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa tunaweza kufanya kazi
nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao wasiokuwa na tija.
Mpira ni ajira hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi
inayostahili kwa vijana wetu ili kupunguza tatizola ajira nchini lakini
pia kutumia vipaji vyao kulipa taifa muonekano stahili.
Mamlaka zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua
hatua kali kwa baadhi ya timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili
kulinda heshima ya mchezo huo bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu
hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014
إرسال تعليق