
Aidha, katika kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi wa
kujitegemea kwa kidato cha nne na sita na wale wa masomo ya maarifa
yanakuwa bora, Serikali imekasimisha jukumu la kudhibiti vituo
vinavyotoa masomo kwa Taasisi ya Elimu Tanzania.
Akizungumza jana na
waandishi wa habari, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa alisema pamoja na mfumo wa alama kubadilika kutoka alama tano
za miaka ya nyuma na kufikia alama saba, haijabadilisha kitu .
"Tumeongeza
alama ili kuwatenganisha wanafunzi, lakini hii haijabadili kitu
chochote, hivyo sifa za kuingia kidato cha tano zitakuwa ni daraja la
kwanza hadi daraja la tatu," alisema.
Baada ya Serikali kuongeza
alama za viwango, kutoka alama tano za awali (A,B,C,D na F) na kuongeza
alama (A,B+, B, C, D, E na F) wazazi na wanafunzi wamekuwa na dukuduku
la kutaka kufahamu sifa za wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo
.
Daraja kwa kwanza ni pointi 7 -17, daraja la pili pointi 18-24 na daraja la tatu ni pointi 25-31.
Aidha,
akizungumzia kukwamua mwanafunzi wa kujitegemea ambao wameonekana
ufaulu wao kutokuwa mzuri, Kawambwa alisema serikali imeamua kuipa
jukumu TIE kudhibiti na kuhakikisha elimu inayotolewa kwenye vituo hivyo
inakuwa bora na inayomwezesha mwanafunzi kufanya vizuri.
"Kuanzia
mwaka huu, Taasisi ya Elimu Tanzania tumeipa jukumu la kukagua vituo na
kuangalia elimu inayotolewa, na tutaendelea kuboresha mazingira kila
wakati ili ufaulu wa wanafunzi hawa uwe mzuri," alisema.
Wakati huo
huo, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI
inatarajia kuadhimisha Wiki ya Elimu ambayo pamoja na mambo mengine
itatumika kutoa motisha na zawadi kwa shule na wanafunzi waliofanya
vizuri kwa matokeo ya shule ya Msingi na Kidato cha Nne 2013.
إرسال تعليق