Wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamuunga mkono JK

 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamempongeza na kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ufafanuzi na kuunga mkono hotuba yake kwa Bunge la Katiba aliyoitoa tarehe 21 Machi, Mjini Dodoma.

Wazee hao wamefika Ikulu ya Dar es Salaam leo jioni , tarehe 9 Aprili,2014  na kuelezea furaha yao kwa Rais Kikwete.
“Wazee wote tunakushukuru, tumefurahishwa sana na Hotuba ile kwani umetoa ufafanuzi wa mambo mengi, kwa hivyo tumefika hapa kukufahamisha kuwa tumefurahishwa sana, tuko pamoja nawe kwa hali ya aina yeyote “ wamesema na kumueleza Rais kuwa wanayo mabaraza katika Wilaya, Mikoa, Kata na hata Mashina.

“Tumefurahi sana , hotuba hii imetufungua na tumefunguka  hivyo tunakuunga mkono na tuko nawe katika hoja ya Serikali mbili kama ilivyo katika Chama Chetu.” Wazee hao waliongozwa na Bi. Khadija Jabir Mohammed ambaye ndiye kiongozi wao na Bw. Waziri Mbwana Ali Katibu wa Wazee. Wazee wengine  waliofika Ikulu ni  Bw. Juma Ame Juma, Bw. Mohammed Khamis Haji, Bw.  Juma Khamis Khamis na  Bw. Tabib Omar Makungu.  Wengine ni Alchui Khamis Alchui, Bw. Abdallah Rashid Abdalla na Bw. Haji Machano Haji.

Rais amewashukuru Wazee hao kwa kumtia moyo kwa kufika Ikulu kuelezea hisia zao ambapo Rais amewaeleza Wazee hao kuwa takwimu zote alizotumia katika Hotuba yake amezitoa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Warioba na kwamba hata maswali aliyokuwa akiuliza, alikuwa akiyauliza kwa nia ya kuyatafutia majibu na majawabu ya misingi kama yalivyoandikwa kwenye rasimu ya Tume.



“Takwimu zote nimetoa kwenye taarifa ya Tume, Maswali niliyouliza nimeyatoa kwenye taarifa, pia kuna mambo ya uandishi ambayo hayakuwa yameandikwa sawasawa hivyo nina wajibu wa kutoa tahadhari kwa wajumbe wa tume ili kuwa na uhakika wa dhana na tafsiri zilizomo kwenye rasimu ya Tume” Rais Kikwete amefafanua zaidi.

Mwisho!

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.

9 Aprili, 2014

Post a Comment

أحدث أقدم