WU-TANG CLAN “Secret Album” Yapanda Dau mpaka $5 Million.

wu-tang-clan-performing
The Wu-Tang Clan kundi la muziki wa HIP HOP kutoka mji wa NEW YORK nchini AMERICA ambalo limeunganisha EAST COAST rappers RZA, GZA, Method Man, Raekwon, Ghostface Killah, Inspectah Deck, U-God, Masta Killa na Marehemu Ol’ Dirty Bastard. Kundi hili lilitengenezwa na kuwa na mahusioano na “New York City Borough of Staten Island”, ambapo U-God, Method Man, RZA, Ghostface Killah na Raekwon ambao walikua wananjitambua kama wanachama wa “Shaolin” pamoja na kuwa wanachama wingine walikua wakitoka Brooklyn NY kama marehemu “Ol Dirty Bastard, GZA na Masta Killa na mara nyingi sana walikua wakiungana na rafiki wa utotoni “Childhood Friend” rapper kutoka huko huko America “Cappadonna”.
Wu_Tang_Clan_on_Stage
Baada ya kimya cha muda mrefu kundi la Hip Hop la Wu-Tang Clan’s wameamua kutoa wanachoita “a Secret Album” ambayo ipo tayari kwenye “MNADA” wa kuuzwa mara moja tu ambapo kuna wadau wengi na wakubwa wameishaidandia na kupanda “DAU”, baada ya kusema kuwa wao watauza master copy tu ya album hiyo ijulikanayo kama  ”Once Upon A Time In Shaolin”  itauzwa kwa yule atakaekuja na dau kubwa na kuchukua album hiyo na kuwa ya kwake ambapo mpaka sasa OFA zimekuja kuanzia Dola Milioni Mbili ($ 2 MIILION) na kuna mtu ambae ameahidi kuichukua kwa Dola Milioni Tano ($ 5 Million) ila bado wanaendelea kusubiri kama atatokea MDAU mwingine atakaepanda zaidi ya hapo.
RZA ambae ni kiongozi wa kundi hilo alisika hivi karibuni akizungua na Billboard kuwa:
“Offers came in at $2 million, somebody offered $5 million yesterday. So far, $5 million is the biggest number. I don’t know how to measure it, but it gives us an idea that what we’re doing is being understood by some. And there are some good peers of mine also, who are very high-ranking in the film business and the music business, sending me a lot of good will. It’s been real positive.”
Kundi hili bado halijatangaza rasmi lini wataachia ALBUM hiyo, ila kwa sasa watakua wanaonyesha kazi zao  na kazi yao hiyo (Showcasing the LP in Museums) kwenye Makumbusho mbali mbali, Matamasha (Festivals), Maonyesho (Galleries) duniani kite kabla hawajatangaza lini wataachia album hiyo kwenye Mauzo (SALE)

Post a Comment

Previous Post Next Post