Ya muhimu aliyozungumzia Balozi Mulamula kwa Watanzania, Columbus

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania wa Ohio kwa kuwashukuru kwa makaribisho mazuri waliyompa na kusisitiza upendo na umoja miongoni mwao.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania wa Ohio kwa kuwashukuru kwa makaribisho mazuri waliyompa na kusisitiza upendo na umoja miongoni mwao.

Balozi Mulamula aliwasifu Watanzania wa Columbus kwa jitihada zao za kufanya vizuri kwenye maisha kwa kutimiza malengo yao yaliyowaleta ughaibuni.

Pamoja na kufanya fundraising ya mfuko wa Jumuiya kwa ajili ya kutatua matizo yanayotokea kwenye Jumuiya hiyo, amewaasa kujiandikisha na bima ya WESTADI kwani ni nafuu sana unalipa $300 tu kwa mwaka au kama haiwezekani akashauru kutafuta bima yoyote hata hapa ughaibuni ili kuondoa adha ya michango ya mara kwa mara ambayo wakati mwingine haitimizi malengo na hata kuwa usumbufu kwa wengine. Alitolea mfano kwa Mtanzania ambaye mwili wake ulilazimika kuchomwa moto huko Wisconsin, jambo ambalo siyo utamaduni wetu kwani tumezoea kuzikwa aidha ughaibuni au nyumbani. Shughuli ya mwili kuchomwa moto ni gharama pia, hivyo alisisitiza kuwa "bado ndugu zangu jitahidini muwe na bima." 

Mhe. Balozi Libarata Mulamula vile vile alijibu maswali ya hapo kwa papo. Maswali mengi yaligusa sala la uraia-pacha kwa WanaColumbus kutaka kujua Ubalozi unasaidiaje. Mhe. Balozi aliwajibu kwa kuwafahamisha kuwa suala hilo ni la Wanaughaibuni wote na hivyo hawana budi kuwa kitu kimoja ili waweze kulifanikisha. 

Ubalozini kupitia Wizara wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wamelisimia kidedea lakini akasisitiza kuwa "kikubwa kinachohitajika ni umoja wenu wa kulipa kipaumbele swala zima la uraia pacha."

Mhe. Liberata Mulamula akipokewa na mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri mara tu alipowasili kwenye fundraisng dinner ya Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio iliyofanyika Comfort Inn siku ya Jumamosi April 19, 2014.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiingia ukumbini akiwa ameongozana na mweka hazima Bi. Vera Teri.


Mjumbe Michael Mnngodo akiutambulisha uongozi wa Jumuiya kwa Mhe. Balozi Libarata Mulamula na mumewe.

Mjumbe Chiseko Hamisi akielezea mfuko na kazi za mfuko huo na kusisitiza wanajumuiya wajiunge kwa wingi.

Mjumbe Joe Ngwilizi akisoma wasifu wa Balozi Liberata Mulamula.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa katibu wa Jumuiya Bi. Happiness Salukele.

Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri.


Meza kuu kutoka kushoto ni katibu wa jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James.

Watanzania waliohudhuria fundraising dinner.
Picha na maelezo kutoka kwa Luke Joe/Vijimambo blog

Post a Comment

Previous Post Next Post