Mazishi ya muongozaji na msanii wa filamu Adam Kuambiana
yatafanyika Jumanne (May 20) katika makaburi ya Kinondni jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza, mwenyekiti wa bongomovie ,Steve Nyerere
amesema kuwa marehemu ataagwa Leaders Club siku hiyo hiyo kabla ya
mazishi.
“Habari za mazishi ni kwamba atazikwa siku ya jumanne na tutazika
katika makaburi ya Kinondoni, kuagwa ataagwa siku hiyo hiyo katika
viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 na baada ya
hapo tutaelekea kwenye makaburini,” alisema.
Pia Steve Nyerere amedai kuwa marehemu Adam Kuambiana alikuwa na
matatizo ya tumbo ambayo ndo yadaiwa chanzo cha kifo chake. “Marehemu
alikuwa nasumbuliwa na tumbo tu, yani alikuwa anasumbuliwa na vidonda
vya tumbo na hivyo ilivyotokea.”

Post a Comment