Na Mwandishi Wetu
KASSIM Dewji anayeaminika ni katibu mkuu mwenye mafanikio ya juu zaidi katika Klabu ya Simba, ameibuka na kutoa siri kuwa kuna viongozi waliuza viwanja viwili mali ya klabu hiyo.
KASSIM Dewji anayeaminika ni katibu mkuu mwenye mafanikio ya juu zaidi katika Klabu ya Simba, ameibuka na kutoa siri kuwa kuna viongozi waliuza viwanja viwili mali ya klabu hiyo.
Dewji aliyeiongoza Simba kuitoa Al Ahly mwaka 2003, amesema Simba
ilikuwa na viwanja vinne katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam,
lakini viongozi waliokuwa madarakani miaka ya 1980, waliviuza.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Dewji alisema
alifanya uchunguzi wakati akiwa katibu mkuu na kugundua suala hilo
kwamba ilifanyika hujuma.
“Baada ya hapo nikalazimika kutafuta mwekezaji kwa ajili ya kujenga
kile kiwanja kingine ambacho kilikuwa wazi na yamewekwa makontena tu.
Pia tayari jiji lilianza kutishia kukipora kwa madai kuwa hakiendelezwi.
“Jengo ambalo mwekezaji alilijenga ndiyo lile lenye maduka,
linajulikana kama Jengo la Dewji na linaiingizia Simba shilingi milioni
180 kwa mwaka,” alisema.
Akizungumzia uchaguzi wa Simba, Dewji alisema hataki kumpigia mtu kampeni badala yake anawaasa Wanasimba kuwa makini zaidi.
Akizungumzia uchaguzi wa Simba, Dewji alisema hataki kumpigia mtu kampeni badala yake anawaasa Wanasimba kuwa makini zaidi.
“Wanasimba wanajua nani wamchague, lakini lazima wawe makini na waangalie watu wanaowachagua huko nyuma wamefanya nini.
“Maana wengine wana kesi, hawakuwa waadilifu au walikwama kwenye
taasisi walizokuwa wanaziongoza. Wasiruhusu waingie na kuivuruga Simba,
kweli kabisa kama wanahitaji msaada wangu, mimi nipo ingawa msitegemee
kuwa ninataka uongozi,” alisema.
Dewji alisisitiza kukubali viongozi wasio waadilifu kuchukua madaraka Simba ni sawa na kuiangamiza kwa miaka mingine minne ijayo.
Dewji alisisitiza kukubali viongozi wasio waadilifu kuchukua madaraka Simba ni sawa na kuiangamiza kwa miaka mingine minne ijayo.

Post a Comment