Dr. Dre yupo njiani kuwa rapper wa kwanza BILLIONAIRE pale kampuni ya Apple itakapoinunua kampuni yake yake Beats Electronics.

Kwa mujibu wa TMZ, Apple inadaiwa itainunua Beats kwa gharama ya
$3.2 BILLION. Dre na mwanzilishi wa Interscope, Jimmy Iovine ndio
walioanzisha kampuni hiyo. Dre na Jimmy walianzisha kampuni hiyo mwaka
2008 kwa kutengeneza headphone lakini sasa wanatengeneza pia spika,
vifaa vya sauti vya kwenye magari na mtandao wa kustream muziki.
Deal hiyo inaweza kukamilika wiki ijayo na itakuwa deal kubwa zaidi
ya kampuni Apple. Dre alikamata nafasi ya pili kwenye orodha ya Forbes
ya wasanii wa hip hop matajiri zaidi akiwa na $550 million nyuma ya
Diddy mwenye $700 million.
Post a Comment