Mwaka huu tuzo za muziki za Kilimanjaro hazijawa na malalamiko
kwenye vipengele vingi kama ilivyokuwa miaka iliyopita. Pamoja na
Diamond kuzoa tuzo zote saba alizotajwa, ni ushindi wa Fid Q pekee ndio
ulioshangiliwa na tu wengi zaidi.
Sababu ni kwamba pamoja na rapper huyo ambaye jina lake ni Fareed
Kubanda kuaminika kwa wengi kuwa ndio mwandishi hatari zaidi wa mashairi
ya Hip Hop, alikaa miaka 7 bila kupata tuzo yoyote.
Ndio maana katika mahojiano niliyofanya naye, Fid alisema ushindi
wake mwaka huu ni sawa na saa iliyopoteza majira kupatia muda na kwamba
kitu kizuri katika kushinda tuzo ni pale kila mtu anapofurahi, na ndivyo
ilivyokuwa kwake.
Hata hivyo, ni katika kipengele kimoja tu, watu wengi wanaonesha
kutoridhika na mshindi, nacho ni kile cha mtayarishaji bora wa muziki wa
kizazi kipya ambacho kilienda kwa Man Walter. Wengi wanasema producer
huyo hakustahili.
Na kama ulikuwepo ukumbini siku ya utoaji wa tuzo hizo, utakubaliana
name kuwa baada ya jina lake kutajwa, ni watu wachache mno
walioshangalia tofauti na ilivyokuwa kwa washindi wengine. Mbaya zaidi,
kutokana na furaha nyingi kumjaa, producer huyo alijikuta akifunguka
maneno mengi ya furaha hadi ukumbi ukaanza kumzomea na akazimiwa kipaza
sauti.
Ushindi huo, ulimuumiza producer wa wimbo wa Diamond, My Number One, Sheddy Clever aliyeandika:
“Ndugu zangu hivi nitashindwa vp kuchukua tuzo ya producer bora wa mwaka wakati nimetayarisha wimbo uliochukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka na ni wimbo ambao umemfanya Msanii @diamondplatnumz aweze kuchukua tuzo zaidi ya 5 #ktma hii inaonesha kua muziki we2 watanzania bado unahitaji elimu ya kutosha ila cna maana mbaya hapana bt nawashukuru saaana #ktma kwa kazi walio fanya pia.”

Kilio chake kiliungwa mkono na producer mkongwe nchini, Master J aliyesema;
“Sijaelewa Diamond kupata tuzo 7 halafu produza wake kutoka na 0.”
“Sijaelewa Diamond kupata tuzo 7 halafu produza wake kutoka na 0.”
Wengi wanaomuunga mkono Sheddy, wanaamini kuwa ili hesabu ikamilike
vizuri, ushindi wa tuzo saba wa Diamond ulikuwa ni tiketi ya moja kwa
moja kwa producer wake kuchukua tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki.
Hata hivyo producer wa Transorfmax, Lucci alidai kuwa, hit moja pekee
isingetosha kumfanya Sheddy achukue tuzo hiyo.
“Kama producer mwenzako wacha nikuelimishe kidogo mdogo wangu,” Lucci alisema.
“Kwanza, kamwe hujawahi kunisikia mimi nikilalamika kwamba sijapata hata nomination moja kwenye kili awards pamoja na kufanya hits zote kubwa za Cpwaa..Kwanini? kwasabubu it takes more than just a hit song…its takes consistency brother. Watu waone hujabahatisha…kama ningefanya hits zote za Cpwaa ndani ya mwaka moja halafu nisiingie kwenye category hapo sawa, ila kwa nyimbo moja tu au mbili kwa mwaka bado haitoshi. I did Jikubali ambayo ilikua ni kama anthem (ukiacha Ngololo) lakini hata nomination haijapata but hatujapiga kelele. Kwanza shukuru Mungu sana you were even a nominee. Yes production matters kwenye ubora wa wimbo tena sana sana sana lakini, tafakari mwenyewe moyoni mwako je; what made “Number one” a huge hit…was it your production zaidi au Diamond’s establishment as an artist and the love kila mtu aliyonayo kwake? Jibu ni lako wewe na Mungu wako…anyway…hongera walao kwa nomination uliyopata pamoja na kua mpya kwenye game..big up Sheddy.”

Naye mtangazaji wa Magic FM, Salma Msangi alidai kuwa yaliyomtokea
Sheddy ndiyo yaliyowahi kumtokea Man Walter kipindi 20 Percent
aliponyakua tuzo tano kwa mpigo.
“Hata kipindi alichopata tuzo 5 20% Man water hakupata. . So producer wa wakati huo hakustahili #Historia Imejirudia,” alitweet mtangazaji huyo.
Pamoja na Sheddy Clever na Man Walter, wengine waliokuwa
wakishindania kipengele hicho ni pamoja na Nahreel, Marco Chali na C9.
Ni nani sasa alistahili kuwa mtayarishaji bora mwaka huu?
Kwa mtazamo wangu (ambao sio lazima uwe sahihi)
ukiangalia sababu kama idadi ya hits alizofanya, ubora wa nyimbo zenyewe
kwa maana ya kiufundi zaidi, Nahreel alistahili kushinda mwaka huu.
Nahreel ni producer wa miaka mingi na aliyetengeneza hits nyingi sana
lakini ni mwaka jana ndipo alipokuwa amesettle zaidi kufanya kazi hiyo
baada ya kuwa huru kutokana na kumaliza masomo yake nchini India.
Nahreel ni producer aliyekamilika na mwenye uwezo mkubwa wa
kutengeneza nyimbo za aina mbalimbali. Wengi walikuwa wakimfahamu kwa
beat zake za Hip Hop zaidi, zikiwemo zile alizomtengeneza Joh Makini
miaka kadhaa iliyopita mfano ‘Copy My Motion’.
Kwa mwaka jana, Nahreel alitengeneza hits zikiwemo za ‘Nje ya Box’ na ‘Bei ya Mkaa’ za Weusi, nyimbo za kundi lake la Navy Kenzo ukiwemo ‘Chelewa’ na ‘Hold Me Back’, ‘Come Over’ ya Vanessa Mdee, ‘Ball Player’ ya Izzo B aliyowashirikisha Ngwair na Quick Rocka na ‘Love Me’ ya Izzo aliowashirikisha Barnaba na Shaa.
Hizo ni baadhi tu ya nyimbo alizozitengeneza mwaka jana mkali huyo
ambazo hakuna anayeweza kubisha kuwa zilihit ile mbaya. Mkusanyiko wa
nyimbo hizo ndio unaozalisha sifa ya kuwa ‘consistency’ aliyoisema Lucci kwenye mtazamo hapo juu.
Pengine ili kuona ukali wa Nahreel, ni bora kuzifahamu pia hits alizozifanya mwaka huu ambazo ni pamoja na ‘Gere’ ya Weusi, ‘Mfalme’ ya Mwana FA f/ G-Nako, My Papa ya Feza Kessy.
Hivyo pamoja na kwamba kura nyingi zilimwendea zaidi Man Walter, kwa mtazamo wangu ni Nahreel ndiye aliyekuwa anastahili kushinda mwaka huu. Nyimbo pekee za Man Walter zilizofanya vizuri mwaka jana ni ‘Yahaya’ na ‘Joto Hasira’ za Lady Jaydee na ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz’ (ambayo aliitengeneza kwa kushirikiana na Marco Chali).
Kwahiyo kwa idadi ya hits zilizofanyika mwaka jana, Nahreel alikuwa
nazo nyingi zaidi kumzidi Man Walter. Hata hivyo katika masuala ya tuzo
hasa yanayohusisha upigaji kura, hilo linaweza lisiwe kigezo na kura za
wananchi ni muhimu ziheshimiwe. Wananchi ndio walioona Man Walter ni
producer bora wa mwaka jana.
Post a Comment