ARSENAL YASHINDA 1-0

KLABU ya Arsenal imerudi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa bao 1-0 jana jioni dhidi ya West Brom Uwanja wa Emirates, London.
Na kwa kipigo cha Everton jana kutoka kwa Manchester City, The Gunners tayari wamejihakikishia kucheza kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Olivier Giroud alifunga bao hilo pekee dakika ya 14 likiwa la 22 msimu huu, Arsenal ikiibuka na mabadiliko makubwa katika kikosi cha kwanza kutoka kile kilichofungwa na Newcastle Jumatatu, Mathieu Flamini akichukua nafasi ya Aaron Ramsey, ambaye alipumzishwa kwa sababu majeruhi.
Olivier Giroud akishangilia bao lake pekee lililoipa Arsenal ushindi wa 1-0
Arsenal sasa inatimiza pointi 76 baada ya kucheza mechi 37 na inaendelea kubaki nafasi ya nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 79 za mechi 37, Manchester City pointi 80 za mechi 36 na Liverpool pointi 80 za mechi 36 pia.

Post a Comment

Previous Post Next Post