Kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Rapper Tupac Omar Shakur 1996, polisi
aliefika katika tukio dakika chache kabla ya Tupac kufariki kufariki
amesema alichokiongea Tupac.
Katika interview na Vegas Seven hivi karibuni, polisi ofisa wa kwanza
kufika katika tukio la kifo cha Tupac 1996 ameongea kuhusu maneno ya
mwisho yaliyotolewa na Tupac kabla ya kufariki.
Chris
Carroll, ofisa wa zamani wa kitengo cha Las Vegas Metropolitan amesema
kuwa alipokea simu juu ya tukio la risasi lililotokea karibu na makutano
ya Flamingo na Koval mida ya saa 11:15 usiku ambapo alikuwa mwenyewe.
Kutokana na
maelezo ya Carroll alipofika katika eneo la tukio na kujaribu kumtaka
Tupac kumtaja aliempiga risasi, Tupac alikuwa busy kumkalipia Suge
Knight
"Ninamuangalia
Tupac, nae anajaribu kumkalipia Suge , na nnamuuliza, nani amekupiga
risasi? nini kimetokea? nani kafanya hivi?, lakini alikuwa
akiinipuuzia.alikuwa akiniangalia hapa na pale, lakini anajaribu
kumkalipia Suge
Nikaendelea
kumuuliza tena na tena, nani kafanya hivi? nani kakupiga risasi? na
akaendelea kunipuuzia, kisha nikaona katika uso wake, katika movement
zake, ghafla akabadilika, akaacha kuhangaika na kuanza kuongea bila
ushirikiano akisema "niko katika amani" kitu kama hicho, hibyo tu"
Carroll baadae alielezea maneno ya mwisho aliyoyasema Tupac kabla ya kuanza kukukuruka na kuzimia.
"Aliniangalia
na kuvuta pumzi kujaribu kutoa maneno, na akafungua mdomo wake
nikidhani ntapata ushirikiano wake, lakini maneno yaliyotoka ni F***
You."
إرسال تعليق