•Azam TV kurusha “live”
Bingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2013/2014 timu ya Azam FC itakabidhiwa kitita chake cha zawadi Sh 75 Milioni Mei 27 mwaka huu kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi nchini ya Vodacom.

Aidha, pamoja na Azam fc, Vodacom itakabidhi pia zawadi za fedha kwa
Yanga, Mbeya City na Simba waliomaliza msimu katika nafasi ya pili hadi
ya nne.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema tayari
maandalizi ya tukio hilo litakalohusisha chakula cha jioni
yameshakamilisha kwa kiasi kikubwa na kinachoendela sasa ni maandalizi
ya mwisho ikiwemo kusambaza mialiko.
Mwalim amesema tukio hilo hilo litafanyika kwenye ukumbi wa JB
Belmonte uliopo kwenye jengo la Golden Jubilee jijini Dar es salaam na
kuwataka washabiki wa soka nchini kuaka mkao w akuhushudia tukio kubwa
na la aina yake.
“Sasa tunatangaza rasmi kuwa Azam pamoja na timu na wachezaji wengine
waliofanya vema katika maeneo mbalimbali wanaostahili kupata zawadi za
fedha kutoka kwa mdhamini kuwa litafanyika Mei 27. Hii inafuatia
kujiridhisha na maandalizi yote yanayohitajika.”
Mwalim amesema kuwa tukio hilo litarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha AZAM ambao nao kwa upande wao wameshakamilisha maandalizi ya kiufundi kwa kiasi kikubwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa tukio hilo kurushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Mwalim ametoa rai kwa wahusika wote ambao watapokea mialiko ya
kuhudhuria tukio hilo ikiwemo wanaopokea zawadi na wageni waalikwa
kutokosa kwani Vodacom imejipanga kuweka rekodi katika matukio ya aina
hiyo.
“Tunatambua kuwa wadau wa soka wanatamani kuona matukio ya kukabidhi
tuzo/fedha za kimichezo yenye hadhi na viwango vya hali ya juu kama
ilivyo kwa matukio ya ligi za Ulaya na kwengineko duniani, hivyo
tumejipanga kuanza kuleta mapinduzi kwenye Ligi Kuu Vodacom kuanzia
mwaka huu.”
Hata hivyo Mwalim amesema pamoja na wao kujipanga kuwatimizia wadau wa soka nchini ndoto hiyo bado mchango wa wadau wenyewe kufanya tukio hilo kuwa la aina yake ikiwemo wale wote wanaoalikwa kuhakikisha wanafika hususan walengwa wa zawadi.

“Tunaweza kufanya kila kitu lakini kama tukio lenyewe ni la tuzo na
wale tunawaoaalika ama kualikwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ama
Bodi ya Ligi kwa kutambua kuwa wamo katika orodha ya wapokeaji zawadi
hawafiki kwenye tukio ni wazi italeta pengo na kasoro kubwa inayoweza
kuharibu maandalizi yoye mazuri yaliyofanywa.”
Mwalim amayataja maandalizi yaliyokuwa yakisubiriwa kuwa ni pamoja na
kukamilika kwa mchakato wa upatikanaji majina ya wachezaji na timu
zinazostahili kupokea zawadi, maandalizi ya kiufundi kutoka Azam TV
pamoja na kupisha baadhi ya matukio mengine makubwa ndani ya Vodacom
ikiwemo uzinduzi wa huduma mpya ya M-pawa mabyo imefanyika juzi.
Mwalim ameseam kuwa kurushwa moja kwa moja kwa tukio hilo kwenye TV kutanogesha tukio zima kwani kutatoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kushuhudia ama timu zao au wachezaji wanaowashabikia wakipokea zawadi zao.

Mwalim amesema kurushwa moja kwa moja kwa tukio hilo kunaendana na
mambo mengi mazuri ambayo AZAM TV wanatarajia kuyarusha ukumbini na hata
kwa watazamaji watakaofuatilia utoaji huo wa tuzo hizo ikiwemo rekodi
za matukio mahiri ya wachezaji, vilabu na hata mashabiki kwa mechi za
msimu wa 3013/2014
Mwalim amewapongeza AZAM TV kwa kukubali kwao kuwa mbia kwenye tukio
hilo katika eno la matangazo na utayarishaji wa matukio ya kimichezo.
“Tunawapongeza na kuwashukuru AZAM TV kwa kukubali kuungana nasi kwenye tukio hilo, Vodacom ina amini kuwa maendeleo ya mpira wa miguu nchini yanahitaji ushiriki na mchanago wa wadau wengi zaidi na ndio maana wakati wote tumeweka milango ya udhamini wazi kwa wadau wanaopenda kufanya hivyo bila kuathiri vipengele vya msingi vya mkataba mkuu.”

Mwalim amewashukuru TFF na Bodi ya Ligi kwa ushirikiano wao mkubwa
uliofanikisha kukamilka kwa maandalizi ya tukio hilo la utoaji zawadi na
tuzo, ushirikiano ambao amesema unaendelea kuleta tija kwa familia ya
mpira wa miguu hapa nchini hususan ligi kuu ya Vodacom.
Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.
Wengine watakaovuna fedha kutoka Vodacom ni timu iliyoonyesha nidhamu (Sh. 16), mchezaji bora (5.2M), mfungaji bora (5.2M), mlinda mlango bora 5.2M), mwamuzi bora na mwalimu bora 7.8M kila mmoja

إرسال تعليق