Mwili
wa Balozi huyo uliyosafirishwa na Serikali ya Tanzania, uliwasili jana saa 5:45
mchana (kwa sasa za Tanzania) katika kiwanja cha ndege cha Chileka, Blantyre na
kupokelewa na Rais wa Malawi, Dk Joyce Banda aliyelazimika kukatisha kampeni za
kugombea urais ili kushiriki katika tukio hilo la majonzi.
Kulikuwa
na mamia ya ndugu na marafiki waliofika katika uwanja huo wa kimataifa ili
kumpokea mpendwa wao. Malawi inafanya uchaguzi mkuu Mei 20 ambapo Rais Banda
anakabiliwa na upinzani wa wagombea urais wengine 11.
Akiongea
katika hafla fupi ya kupokea mwili wa Balozi huyo, Rais Banda alimshukuru Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania kwa kuchukua jukumu la kusafirisha mwili wa
Chidyaonga hadi nyumbani na kuonesha ushirikiano mkubwa.
“Rais
Kikwete alinipigia simu baada ya kupata habari za msiba. Tena hakuwa nchini
mwake lakini akaonja ni vyema anijulishe. Nilimwambia basi tutafanya utaratibu
wa kuleta mwili wa balozi nyumbani, lakini akasema hilo litakuwa jukumu lake,”
alisema na kumshukuru kwa niaba ya wana Malawi.
Alisema
Balozi Chidyaonga ndiye aliyemshawishi kuhudhuria katika sherehe za miaka 50 ya
Muungano wa Tanzania na Zanzibar akimwambia ilikuwa ni muhimu ashiriki sherehe
hizo akiwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Naye
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema
katika hafla hiyo kwamba Watanzania wanaungana na wenzao wa Malawi kuombeleza
msiba huo wa gahfla wa Balozi Chidyaonga ambaye alimuita kuwa ni ‘Malkia wa
Amani’.
“Alikuwa
Malkia wa Amani na mchapakazi. Baada ya Mkutano wa SADC, Balozi Chidyaonga
aliendeleza mijadala mingi ya amani bila kuchoka,” alisema Waziri Membe na
kuahidi kwamba ujumbe wa Rais Kikwete kwa Wamalawi utasomwa leo wakati wa
mazishi.
Naye
kiongozi wa familia ya balozi huyo, Andrew Machinjire, aliishukuru Tanzania kwa
kuchukua jukumu la kutoa ndege ya serikali ili kusafirisha mwili wa balozi
huyo.
“Kwa
kweli Tanzania imeonesha kwamba siyo tu ni jirani mwema, bali ndugu wa karibu
na mwenye upendo,” alisema.
Post a Comment