BHitz washangazwa na STORY ya Dogo Janja

20140507-190801.jpg
 Sakata la madai ya mwanamuziki wa kizazi kipya ‘Dogo Janja’ dhidi ya Producer ‘Pancho Latino’ umechukua sura nyingine baada ya GongaMX Team kuzungumza na uongozi wa kampuni hiyo jioni hii kutokana na habari ya mchana huu kuhusiana na malalamiko ya msanii huyo kuwa amezungushwa na producer huyo zaidi ya miezi 7 na kusema kuwa alikua hapokelewi simu zake na kutamka kuwa producer huyo ni “Mizinguo”.
Baada ya kuzungumza na Producer Pancho Latino, alisema kuwa habari hizo ni za uongo na wala hajui zimetokea wapi sababu yeye binafsi hammiliki msanii ‘Dogo Janja’ na kazi hiyo alikua amepewa kufanya bure kabisa na hajawahi kukimbia simu za msanii huyo. Producer Pancho Latino alituma kidhibiti cha Dogo Janja kuchat nae na kumwambia aje studio kumalizia nyimbo hiyo na pamoja na kulalamika kuwa hakuwa na nauli ya kufika studio za BHitz kuchukua ngoma hiyo ambayo imemalizika lakini Msanii huyo alilalamika kutokuwa na pesa mfukoni za kumfikisha huko na Producer Pancho Latino alijitolea kwa kumwambia “Azima kwa mtu nitakupa ukija”.
Evidence toka kwa Producer Pancho.
20140507-190112.jpg
CEO wa kampuni ya BHitz ambae naye ni mmoja wa maproducer wakubwa sana na wanaoheshimika hapa nchini ‘HERMY B’ ameshangazwa sana na maneno ambayo Dogo Janja aliyozubgumza kuhusiana na kampuni yake amesema “hata kama tumekuwa na matatizo na wasanii wengine, ndio iwe sababu ya kusingiziwa kila kitu? Is not fair kabisa, Dogo Janja tumemfanyia nyimbo for “Good Will” na wala hajachajiwa chochote na haya yote ambayo amezungumza si ya ukweli kabisa na yanatusababishia matatizo tu wakati hatuna tatizo na mtu yoyote”.

Post a Comment

أحدث أقدم