Mwanamziki “Ciara
Princess Harris” mwenye umri wa miaka 28 amejifungua mtoto wa kiume siku
ya jumatatu May 19, Mtoto huyo ambae babake yake ni msanii “Future”
ambapo wasanii hao wamekuwa wapenzi kwa
muda kidogo. Ciara aliweka picha za mwanae kwenye instagram ikionyesha
mkono wa mwanae mchanga kuonyesha kuwa ameshazaliwa. Ciara aliweka wazi
ujauzito wake mwezi wa January kwenye The View na kuzungumzia ni jinsi
gani alikuwa hawezi kusubiri kupata mtoto huyo ambae kwa sasa ameshakuja
duniani. Hii ni kama vile Beyonce alivyofanya wakati anatangaza
ujauzito wake soon baada ya kuwa Blue Ivy yupo njiani.
“Nayvadius D. Wilburn” aka Future, 30, alitabiri wakati mahojiano
kwenye radio moja huko nchini Uingereza kwamba alikuwa anategemea mtoto
huyo kuwa wa kiume. Ciara na Future walitangaza engagement yao mwezi wa
October baada ya kuwa katika uchumba wa miezi tisa, Future alimvalisha
Ciara pete ya diamond katika weekend ya birthday yake na kufunga pingu
za maisha. Future akiwa ni baba wa watoto wawili na sasa ameongeza wa
tatu na mkewe mwanadada Ciara.
Post a Comment