Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt, Charles Kimei.
Na Nathaniel Limu, Iramba
BENKI
ya CRDB imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja katika
bajeti yake mwaka huu kwa ajili ya kuchangia katika shughuli
mbalimbali za uboreshaji wa huduma za kijamii nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB Dkt, Charles Kimei amesema hayo kwenye hafla ya
kukabidhi visima kwa shule tatu za msingi na sekondari mkoani Singida
vilivyofadhiliwa na benki hiyo.
Dkt.
Kimei amesema fedha zilizotumika kwa shughuli hiyo ni sehemu ya zaidi
ya shilingi bilioni moja ikiwa ni asilimia moja ya faida
inayotengwa na benki hiyo kila mwaka kusaidia huduma za jamii.
Amesema
mwaka jana, benki ya CRDB ilipata faida ya zaidi ya shilingi bilioni
100 hivyo kulazimika kutenga kiasi hicho cha fedha kama ilivyo sera
yake ya kurejesha sehemu ya faida kwa wateja.
Kutokana
na hali hiyo, Dkt. Kimei ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea
kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii
husani maji safi na salama ambayo bado ni changamoto kubwa Vijijini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Yahaya Nawanda, ameishukuru benki
hiyo kwa kufadhili uchimbaji na ujenzi wa visima hivyo husani kwa
shule ya msingi Kizege yenye walemavu wa ngozi ambao walikuwa wakitembea
umbali wa zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma hiyo.
Hata
hivyo watoto hao albino licha ya kushukuru kwa msaada huo wameomba
kuunganishiwa maji hadi kwenye mabweni yao badala ya kulazimika kufuata
nje suala ambalo ni hatari kwa maisha yao.
Pamoja
na kufadhiliwa na CRDB na wadau wengine shughuli za uchimbaji na
ujenzi wa visima katika shule tatu za msingi na sekondari mkoani
Singida zimefanywa na Shirika la Nkwamira.
إرسال تعليق