DIAMOND azidi “KUNG’AA” TUZO za KORA.!

tz
Msanii kutoka nchini Tanzania Nassib Abdul {Diamond Platnumz}, baada ya kutwaa ushindi mkubwa katika tuzo za ‘Kili Music Awards 2014′ za nchini Tanzania, kwa kufanikiwa kunyakua tuzo 7 na kuvunja rekodi alioiweka msanii ‘Twenty Percent’.
Katika Tuzo za KORA msanii huyo imeonekana kuongoza katika nafasi nzuri zaidi kutokana na jina lake limekua likitajwa zaidi na mashabiki katika ukurasa wa Kora facebook. Wiki 17 toka  kura kutoka kwa mashabiki waanze kupiga, Diamond ameonekana kuwashinda wenzake wakubwa kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Fally ipupa, Koffie Olomide, Werason na wengine zaidi.
Hongera Diamond kwankuiweka Tanzania kwenye MAP ya Africa Entertainment.
diam

Post a Comment

Previous Post Next Post