Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, akizungumza kwenye kilele
cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi),yaliyofanyika
kimkoa katika uwanja wa namfua mjini Singida (01/5/2014).Maadhimisho ya
mwaka huu kwa mkoa wa Singida yalihudhuriwa na watumishi wa umma na
wananchi wachache ukilinganisha na miaka iliyopita.Kushoto ni mratibu wa
RAAWU mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kilele cha maadhimisho ya
sherehe ya siku kuu ya wafanyakazi duniani (Mei mosi mwaka huu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida,Dk.Vicent Kone amewahimiza walimu,wazazi na walezi
kuongeza juhudi katika kuwashawishi wanafunzi wengi zaidi kusomea masomo
ya sayansi ili kama si kupunguza basi kulimaliza kabisa tatizo la uhaba
wa walimu wa sayansi.
Dk.Kone
ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha
sherehe za siku kuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) duniani zilizofanyika
kimkoa katika manispaa ya Singida.
Amesema
kumekuwepo na kilio cha muda mrefu cha uhaba wa walimu wa masomo ya
sanyansi katika shule karibu zote za sekondari mkoani na Tanzania kwa
ujumla.
Amesema
mwarubaini wa kulimaliza tatizo hilo ni kushawishi wanafunzi wengi
kusoma masomo ya sayansi ili watakapohitimu warudi kuja kufundisha
katika shule za hapa mkoani.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.(wa tatu kulia) akishiriki
kuimba wito wa mshikamano wa wafanyakazi.Wa kwanza kulia ni Misholi (wa
pili kulia) ni Blandina Marwa wenyekiti wa sherehe za mei mosi mkoa wa
Singida na mratibu wa RAAWU mkoani Singida.
Aidha,Dk.Kone
amewasisitiza wananchi waendelee kuiunga mkono serikali katika
kuimarisha na kuboresha sekta ya elimu nchini hususani katika
kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ya masomo ya
kemia,fizikia na baolojia.
Katika
hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa madeni ya wafanyakazi
wakiwemo walimu ya zaidi ya shilingi 2.2 bilioni,yanaendelea kuhakikiwa
ili yaweze kulipwa.
Kwa
upande wa wafanyakazi katika risala yao wamewaomba wabunge wa bunge la
katiba kupunguza malumbano na kejeli zisizo na tija na badala yake
wazingatie jukumu lililowapeleka bungeni la kuwapatia wananchi katiba
itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo.
“Sisi
wafanyakazi tunapendekeza katiba inayojali zaidi uhuru,usawa na haki
swa ambazo binadamu anastahili kupata na kuepuka matabaka haswa ya
vipato.Kuepuka ubepari kwa kujilimbikizia mali,ukabaila kwa kujichukulia
ardhi kubwa na unyanyaji wa jasho la wafanyakazi na wakulima”,imesema
sehemu ya risala hiyo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya mei mosi,ni ‘utawala bora utumike kutatua kero za wafanyakazi’.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akimkabidhi cheti mfanyakazi bora
wa mwaka huu wa TANESCO mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya kilele cha
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani – Mei Mosi.Pamoja na cheti,
mfanyakazi huyo Ps wa menejaTANESCO makao makuu mkoani Singida, pia
alizawadiwa Tv screen yenye thamani ya shilingi laki nane.
Baadhi
ya viongozi na watendaji wa serikali waliohudhuria kilele cha
maadhimisho ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa
Namfua mjini Singida.Mwenye miwani ni hakimu mfawidhi mkoa wa
Singida,Minde.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Singida,waliohudhuria kilele cha
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi) yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Post a Comment