WENYE BOTI WAOMBWA KUZIPELEKA MTO KILOMBERO AMBAO UMEFURIKA MAJI

Mkuu wa wilaya ya Ulanga akiwa katika moja ya Boti kivukoni siku ya mei mosi katika ziara. ya kukagua hali ya huduma kivukoni.

Wito umetolewa kwa wamiliki wa boat ndogo katika maeneo mbali mbali kuzileta katika mto kilombero ilikutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa Kilombero na Ulanga kutokana na maji kuendelea kuongezeka katika mto Kilombero.
Eneo la barabara lililo kumbwa na maji.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ulanga MH, Francesi  Miti wakati akizungumza na wananchi  wa kivukoni na wasafiri jana katika eneo la kivuko alipofika kuangalia hali ya huduma za usafiri katika mto Kilombero.
Mitti amewataka  wasafiri wote wanaotumia usafiri wa boat zilizopo sasa ambazo ni boti ya sakosi, boti ya halmashauri ya wilaya ya ulanga, boat ya sua, kuvaa maboya ilikuweza kuwa salama zaidi wanapo kuwa katika vyombo hivyo vya usafiri.
Moja ya boti ikipakia wavukaji
Mapema Miti akiwa katika eneo hilo wananchi na wasafiri walilalamikia bei ya boat hizo ambapo mtu mmoja alikuwa akivushwa kwa shilingi 2000 kutoka bei ya kawaida ya shilingi 200 kwa pantoni ya kivuko,ambapo baada ya mazungumzo na wasafirishaji bei imeshuka hadi kufikia shilingi 1500 kwa mtu mmoja, huku mitumbwi ikipigwa marufuku kutoa huduma ya usafiri kutokana na kasi ya maji katika mto kilombero.
Moja ya mtumbwi ukisafirisha viazi, hali hii ya usafiri imepigwa marufuku
Miti aliambatana na kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, kaimu mkurugenzi wa wilaya ya ulanga, mwenyekiti wa chama cha ccm wilaya ya ulanga, viongozi mbalimbali wa serikali na wajumbe wengine wa chama.
 
CHANZO:DJDUKE.COM

Post a Comment

Previous Post Next Post