Kiungo Frank Domayo ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Azam FC.KIUNGO Frank Domayo ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Azam FC hivi karibuni akitokea Yanga ambako alimaliza mkataba wake, ameamua kufunguka sababu ya kuondoka Yanga.
Lakini wakati akifunguka, upande wa pili kumekuwa na vita kubwa ya
kuwania nafasi yake katika kikosi cha Yanga ambapo tayari wachezaji
watatu kila mmoja anajiweka fiti kuchukua nafasi hiyo.
Akizungumzia juu ya kuondoka kwake Yanga, Domayo alisema sababu kubwa
ni kutaka kuendeleza kipaji chake kwa kuwa Azam kuna kila kitu ambacho
mchezaji anahitaji kuwa nacho.
“Mimi ni mchezaji na nimejiunga Azam kwa lengo la kukuza kipaji changu, lakini pia Azam kuna mahitaji yote anayoyahitaji mchezaji.
“Mimi ni mchezaji na nimejiunga Azam kwa lengo la kukuza kipaji changu, lakini pia Azam kuna mahitaji yote anayoyahitaji mchezaji.
“Ninachoomba viongozi na wapenzi wa Azam waniunge mkono ili tuweze
kufanya kazi kwa pamoja kwani bila ya kuwa na mshikamano tutakuwa
hatufanikiwi lengo letu,” alisema Domayo.
Kuhusu wachezaji wanaowania nafasi yake Yanga ni Salum Telela, Omega Seme na Said Juma ambaye amesajiliwa hivi karibuni akitokea Zanzibar.
Kuhusu wachezaji wanaowania nafasi yake Yanga ni Salum Telela, Omega Seme na Said Juma ambaye amesajiliwa hivi karibuni akitokea Zanzibar.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wachezaji hao kila
mmoja alijinadi kuwa ndiye chaguo sahihi la kuziba nafasi ya Domayo
ambaye alikuwa ni kiungo mkabaji.
“Mimi nina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwa sababu najiamini,”
alisema Telela. Upande wa Omega alifunguka: “Nikipewa nafasi nitafanya
maajabu makubwa.”
Akizungumzia hali hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema:
“Tunafurahi kusikia hivyo na hilo ni jambo zuri kwetu, hivyo tunawaombea
wafanye nyema ili waweze kutimiza lengo lao hilo.”
Aidha, imeelezwa kuwa Domayo amenunua gari aina ya Toyota Altezza kwa Sh milioni 13, pia ameagiza nyingine aina ya Toyota Corolla ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya baba yake.
Aidha, imeelezwa kuwa Domayo amenunua gari aina ya Toyota Altezza kwa Sh milioni 13, pia ameagiza nyingine aina ya Toyota Corolla ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya baba yake.
Post a Comment