Wasanii kutoka Zanzibar, AT na Hammer Q ni miongoni mwa wasanii ambao waliwahi kufanya kazi ya muziki wakiwa ndani ya kundi maarufu la muziki wa mduara la Offside Trick.
Wasanii hao ambao hivi sasa wanaendelea kufanya kazi kama Solo
artists wameiambia tovuti ya Times Fm kuwa kuna siri kubwa katika kundi
hilo na kwamba siri hiyo ndio chanzo cha kuvunjika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wasanii hao wamesema kuwa picha
inayowaonesha wakiwa wawili na ikiwa na neno ‘Siri.. loading’ sio wimbo
wa pamoja bali ina maanisha kuna ‘siri’ na ipo siku wataiweka wazi.
“Hiyo kitu siri, ni kwamba kila mmoja ana siri yake ambayo
kaikuta pale. Kila mmoja atapata muda wake siku muafaka kuweza kuelezea,
kwa sababu vile langu limeshakuwa na la kwao limeshatokea kwa hiyo wao
wenyewe watakuwa na vitu vingi vya kuelezea halafu baadae kila mmoja
ataelezea kwa upande wake kwamba ni kitu gani kilichomfika...” AT ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Mimi nakumbuka siku za nyuma nilisema, mimi siongei vitu vingi.
Itafikia siku ntakuja kuongea vitu ambavyo vipo kabisa reality, hivyo
nikivizungumza sitakuja kuonekana mimi nimemuonea Lil Ghetto lakini kwa
sasa hivi bado mapema waache waende. Ndio maana akaenda Hammer Q kafeli
na wengine wameshafeli.
“Sasa kinachofuata...siku nikija kuzungumza mambo yale ambayo
yapo isije kuonekana kama yule bwana mdogo mimi namuonea, isipokuwa ni
reality. Kwa sababu nyumba kwa nje ukiona imepakwa rangi unawezakusema
nzuri lakini aliyekaa ndani ndiye anajua…mimi ipo siku ntakuja kuitoa
hiyo siri, soon tu.” Ameesema AT.
Kwa upande wa Hammer Q ambaye ametoka katika kundi hilo wiki chache
zilizopita alikiri kuwa kuna siri katika kundi hilo lakini hakuwa tayari
kuifichua.
Lakini alieleza kuwa siku akikutana na AT huenda wakazungumza na kukubaliana kuisema siri hiyo.
“Siku tukikutana na AT…kwa sababu yeye mwenyewe ni mtu wa
mishemishe na mimi mtu wa mishemishe kwa hiyo kama tukikutana hivi
tunaweza tukaizungumza kama ikitokea tukakutana pamoja…tunaweza
tukaisema hiyo siri.” Amesema Hammer Q.
Wasikilize hapa wakieleza kwa urefu:
إرسال تعليق