
Afisa
Fedha Mkuu wa Benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (Katikati) akizungumza
na waandishi (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kifedha wa benki hiyo
katika robo ya kwanza ya mwaka ambapo faida ya benki ya kabla ya kodi
imekua kwa asilimia 42 mpaka shilingi bilioni 6.4 ikilinganishwa na
kipindi hicho mwaka jana. Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Bw.
George Shumbusho na kulia Meneja Fedha Mwandamizi Bw. Issa Hamisi.

Afisa
Fedha Mkuu wa Benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (wapili kulia)
akizungumza na waandishi (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kifedha wa
benki hiyo katika robo ya kwanza ya mwaka ambapo faida ya benki ya kabla
ya kodi imekua kwa asilimia 42 mpaka shilingi bilioni 6.4
ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana. Wa kwanza kushoto ni Meneja
Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Bi. Anita Goshashy, Mkuu wa Hazina wa
Benki hiyo Bw. George Shumbusho (wapili kushoto) na kulia ni Meneja
Fedha Mwandamizi Bw. Issa Hamisi.
======== ======= =======
BENKI
ya Exim imepata faida ya shilingi bilioni 6.8 kabla ya kodi katika robo
ya kwanza ya mwaka wake wa fedha, ambayo ni ongezeko la asilimia 42
ukilinganisha na mahesabu ya mapato ya mwaka jana kipidi kama hiki.
“Tunayofuraha
yakuripoti matokeo mazuri katika mwanzo huu wa mwaka,” alisema Ponda,
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim. “Kukua huku kwa mapato kunaonyesha
mafanikio ya hali ya juu ya benki katika vyanzo mbali mbali vya mapato.
Tutaendelea kuboresha utendaji wetu ili kufikia matakwa ya wateja wetu.
Benki yetu inaendelea kwenda katika mwelekeo nzuri. Tunazidi kupiga
hatua katika kufikia malengo yetu. Matokeo tuliyoyapata ya kifedha
katika robo hii ya kwanza ya mwaka yanatupa matumaini makubwa,”
aliongeza Ponda.
Pato
la jumla limeweza kukua hadi shilingi bilioni 12.5 ambayo ni ongezeko
kwa asilimia 27 ukilinganisha na kipindi sawa na hichi mwaka 2013. Pato
litokanalo na tozo na kamisheni limeweza kukua hadi shilingi bilioni 8,
ambayo ni ukuwaji kwa asilimia 37 ukilinganisha na robo ya mwaka jana,
hali iliyosababishwa na kutanuka kwa biashara ya fedha za kigeni.
“Matumizi
ya uendeshaji wa benki yalidhibitiwa na kupanda kidogo kwa asilimia
11.6 mpaka shilingi bilioni 13, yakitokana na uanzishwaji wa gharama za
matawi mapya na motisha za wafanyakazi zikiwa ni jitihada za kuongeza
upatikanaji wa benki kijeografia na kuimarisha shughuli zake. Kwa hivyo, uwiano wa gharama na mapato umeshuka kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 75 iliyopatikana katika robo ya mwaka uliopita mpaka asilimia 64, "aliongeza.
Amana
za wateja zimebaki palepale shilingi bilioni 747 ukilinganisha na robo
ya mwaka uliopita. Jalada la mikopo limerekodi kupanda kwa asilimia 22
ukilinganisha na robo ya mwaka jana mpaka shilingi bilioni 538 pamoja na
mizania ya benki kukua kwa asilimia 10 mpaka shilingi tilioni 1.1.
“Kipaumbele
kikubwa kwetu bado kipo katika jitihada za kuimarisha nafasi yetu
katika soko na kuboresha huduma ili kufikia matakwa ya wateja wetu
kupitia uboreshaji wa shughuli zetu. Mwenendo mzuri wa kuwatosheleza
wateja ni ishara nzuri inayoonyesha kuwa tutafikia malengo yetu kwa
mwaka huu,” alisema Afisa huyo mkuu wa fedha.
Katika mchakato wa kurahisisha
utoaji huduma bora kwa wateja, baadhi ya shughuli kama vile za kufungua
akaunti na uanzishaji zimeweza kuboreshwa zaidi. Uanzishwaji
wa “operesheni ya pamoja” umelenga katika kuongeza msukumo na motisha
katika michakato yote ya kazi ili kuongeza ufanisi zaidi na kuhakikisha
matakwa ya wateja yanafikiwa kikamilifu,” alisema Bw. Ponda.
Katika jitihada za kupambana
na mabadiliko ya mahitaji ya wateja, Benki imeweza kuliunda tawi lake
la Kariakoo kwa namna ya kuwahudumia wateja ambaowanafanya shughuli
zao zaidi ya masaa ya kawaida ya benki na kuruhusiwa kupata huduma za
kibenki kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku. Pia,"Barua
pepe na SMS" zinatoa ujumbe wa papo kwa wateja kuwajulisha mihamala
mbali mbali inayofanyika katika akaunti zao.
Benki
pia imeendelea na jitihada zake za kutanua huduma zake. Benki hivi
karibuni imefungua tawi jipya katika kisiwa cha Anjouni mjini Domoni.
Kituo cha biashara cha kipekee mkoani Arusha, cha tatu katika jiji na
cha 26 nchini kilizinduliwa rasmi katika robo hii. Benki pia inampango
wa kufungua tawi jipya mkoani Tabora ambalo litafanya jumla ya matawi
kuwa 32 nchi nzima. Kulingana na utendaji
mzuri katika robo hii ya kwanza na fursa zilizopo katika uchumi, Benki
ya inalenga kuboresha zaidi utendaji katika robo ikijikita zaidi
katikakampeni za kimauzo na kuongeza ufanisi zaidi.
Post a Comment