Mshiriki wa Big Brother Afrika, 2013 Feza Kessy ameelezea maisha
yake baada ya kuhamia nchini Afrika Kusini atikokea nchini Botswana kwa
mpenzi wake O’neal aliyekuwa mshiriki mwenzake wa BBA.

Feza akiwa na mpenzi wake O’neal
Feza ambaye kwa sasa yupo jijini Arusha kusalimia ndugu zake,ameimbia
255 ya XXL ndani ya Clouds FM kuwa amejikuta akipata mashabiki wengi
nchini Afrika kusini baada kuhamia.
“Sipo Botswana, sasa naishi South Africa nasoma, nafanya part
recording. Kwahiyo najaribu kupita kwenye industry kule ya muziki,ipo
slow kidogo kwangu mimi kwasababu ni Mtanzania obvious. Kwahiyo kuna
mambo mengi najifunza. Lakini nasoma and najaribu kurekodi kule, nasomea
Community Development. It’s something kipo kwenye my heart. I think ni
something ambacho kitanisaidia itasaidia pia jamii yangu. Nilienda chuo
cha kwanza nikashindwa kuendelea kwasababu ilikuwa ni vurugu pale
nilabidi nihamie kwenye college ndogo ambayo ina watu wachache kwasababu
kule mpaka sasa hivi sio kama bongo watu just wakikuona wanakushangaa
wanakuomba autograph kwahiyo ikawa nimelose focus. So sasa hivi ni
kwenye kingine sipendi kutaja taja. Siku aa kabisa yani siku mbili
nikaona hali inaendelea vilevile watu kuja kushangaa hata sikujua wame
nirecognize vipi. Kwahiyo nikaona ‘heeh hata walimu pia ilikuwa inaleta
kama kama kero fulani,” amesema.
Kuhusu album yake, Feza amesema|:
“Natarajia album yangu itoke mwishoni mwa mwaka huu. So mimi ni
Mtanzania nataka ni represent Tanzania lakini at the same time Africa
nzima inanitambua sasa hivi na hii ni opportunity nzuri ya kuutoa muziki
wa Tanzania nje ili ujulikane. So for me najaribu kubalance Tanzania,
Kenya,Uganda ,West Africa na South Afrika. Kwa sasa hivi nafanya kazi
mwenyewe. Na yeye (O’neal) yupo South Africa anaanza kazi very soon huko
huko Afrika Kusini kwenye radio, ni radio presenter.”
Post a Comment