Feza asimulia maisha ya South, adai alihama chuo alichokuwa akisoma kutokana na watu kumshangaa .


Mshiriki wa Big Brother Afrika, 2013 Feza Kessy ameelezea maisha yake baada ya kuhamia nchini Afrika Kusini atikokea nchini Botswana kwa mpenzi wake O’neal aliyekuwa mshiriki mwenzake wa BBA.
Feza
Feza akiwa na mpenzi wake O’neal
Feza ambaye kwa sasa yupo jijini Arusha kusalimia ndugu zake,ameimbia 255 ya XXL ndani ya Clouds FM kuwa amejikuta akipata mashabiki wengi nchini Afrika kusini baada kuhamia.
“Sipo Botswana, sasa naishi South Africa nasoma, nafanya part recording. Kwahiyo najaribu kupita kwenye industry kule ya muziki,ipo slow kidogo kwangu mimi kwasababu ni Mtanzania obvious. Kwahiyo kuna mambo mengi najifunza. Lakini nasoma and najaribu kurekodi kule, nasomea Community Development. It’s something kipo kwenye my heart. I think ni something ambacho kitanisaidia itasaidia pia jamii yangu. Nilienda chuo cha kwanza nikashindwa kuendelea kwasababu ilikuwa ni vurugu pale nilabidi nihamie kwenye college ndogo ambayo ina watu wachache kwasababu kule mpaka sasa hivi sio kama bongo watu just wakikuona wanakushangaa wanakuomba autograph kwahiyo ikawa nimelose focus. So sasa hivi ni kwenye kingine sipendi kutaja taja. Siku aa kabisa yani siku mbili nikaona hali inaendelea vilevile watu kuja kushangaa hata sikujua wame nirecognize vipi. Kwahiyo nikaona ‘heeh hata walimu pia ilikuwa inaleta kama kama kero fulani,” amesema.
Kuhusu album yake, Feza amesema|:
“Natarajia album yangu itoke mwishoni mwa mwaka huu. So mimi ni Mtanzania nataka ni represent Tanzania lakini at the same time Africa nzima inanitambua sasa hivi na hii ni opportunity nzuri ya kuutoa muziki wa Tanzania nje ili ujulikane. So for me najaribu kubalance Tanzania, Kenya,Uganda ,West Africa na South Afrika. Kwa sasa hivi nafanya kazi mwenyewe. Na yeye (O’neal) yupo South Africa anaanza kazi very soon huko huko Afrika Kusini kwenye radio, ni radio presenter.”

Post a Comment

أحدث أقدم