Fid Q aeleza kwanini maneno yalimuishia kwenye KTMA, aingia jikoni kuwaandalia zawadi mashabiki wake (Audio)

Fid Q ni msanii mwenye maneno mengi (ya busara) kila unapokutana naye, lakini usiku wa Jumamosi katika tuzo za Kilimanjaro, maneno yalimuishia.
Fid q Fid Q akishuhudia tuzo za KTMA 2014
Fid ambaye katika usiku huo alinyakua tuzo mbili, ameiambia Bongo5 kuwa furaha aliyokuwa nayo siku hiyo ingemfanya aongee maneno ambayo bila kutarajia yangeweza kuwakwaza wengine ndio maana hakuwa na maneno mengi.
“Nilikuwa speechless kwasababu nilikuwa najiuliza katika kuongea niseme kwamba ‘leo saa mbovu imepatia majira’ nikaona labda kwamba nimewadisrespect. Kwahiyo nikawa sijui kitu kipi cha kuongea kwasababu kauli nyingi zilikuwa zinakuja ni kama za jamii hiyo ‘saa mbovu imepatia majira’ na kauli nyingine, kwahiyo nikaamua niwe speechless tu kwanza,”amesema Fid Q.
Fid amesema anafahamu kuwa ana mashabiki wengi ambao baada ya kushangilia ushindi wake wanangojea awape ngoma mpya ndio maana ameamua kuingia upya studio kuwaandalia zawadi wanayostahili.
“Aisee sijawahi kupata wakati mgumu kama huu,” amesema Fid. “Nimeingia kwenye library yangu kila ninachosikia naona hapana, naona kama hawatu wanahitaji niandike kitu kingine kipya na sio kutoka kwenye library.”
Fid amewashukuru mashabiki wake waliomwezesha kupata tuzo hizo na amesema anaziona kama baraka.
“Unajua kama alivyosema Buster Rhymes ni kwamba ‘the best thing about winning an award is’ pale unashinda na unaona watu wote wamefurahi.”
Msikilize zaidi hapa.


Post a Comment

Previous Post Next Post