Fid Q ni msanii mwenye maneno mengi (ya busara) kila unapokutana
naye, lakini usiku wa Jumamosi katika tuzo za Kilimanjaro, maneno
yalimuishia.
Fid Q akishuhudia tuzo za KTMA 2014
Fid ambaye katika usiku huo alinyakua tuzo mbili, ameiambia Bongo5
kuwa furaha aliyokuwa nayo siku hiyo ingemfanya aongee maneno ambayo
bila kutarajia yangeweza kuwakwaza wengine ndio maana hakuwa na maneno
mengi.
“Nilikuwa speechless kwasababu nilikuwa najiuliza katika kuongea
niseme kwamba ‘leo saa mbovu imepatia majira’ nikaona labda kwamba
nimewadisrespect. Kwahiyo nikawa sijui kitu kipi cha kuongea kwasababu
kauli nyingi zilikuwa zinakuja ni kama za jamii hiyo ‘saa mbovu imepatia
majira’ na kauli nyingine, kwahiyo nikaamua niwe speechless tu
kwanza,”amesema Fid Q.
Fid amesema anafahamu kuwa ana mashabiki wengi ambao baada ya
kushangilia ushindi wake wanangojea awape ngoma mpya ndio maana ameamua
kuingia upya studio kuwaandalia zawadi wanayostahili.
“Aisee sijawahi kupata wakati mgumu kama huu,” amesema Fid.
“Nimeingia kwenye library yangu kila ninachosikia naona hapana, naona
kama hawatu wanahitaji niandike kitu kingine kipya na sio kutoka kwenye
library.”
Fid amewashukuru mashabiki wake waliomwezesha kupata tuzo hizo na amesema anaziona kama baraka.
“Unajua kama alivyosema Buster Rhymes ni kwamba ‘the best thing about
winning an award is’ pale unashinda na unaona watu wote wamefurahi.”
Msikilize zaidi hapa.
إرسال تعليق