Msanii wa muziki, Rehema Chalamila aka Ray C amelazwa katika
hospitali ya Mwananyala wodi namba tano kutokana na ugonjwa wa Dengue
Ray C akiwa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala
Ray C akiwa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala
Akizungumza na gazeti la Mwananchi ,Daktari ambae alikataa kutajwa
jina lake,alithibitisha kulazwa kwa Ray C kutokana na ugonjwa huo jana.
“Tumethibitisha kwamba Ray C ana dalili zote za dengue, lakini kimaadili
siruhusiwi kutoa taarifa za mgonjwa,” alisema daktari huyo ambaye
hakutaka kutajwa jina lake. Hata hivyo,kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi
limethibitisha kumwona mwanamuziki huyo hospitalini hapo akiwa katika
usingizi mzito na madaktari walisema hakuwa katika hali mbaya bali
alikuwa amelala kwa sababu ya uchovu wa dawa.
Mbali na Ray C, pia madaktari watatu na muuguzi mmoja wameripotiwa kuugua ugonjwa huo.
Tayari mamlaka zimetoa tahadhari kwa wananchi kuwataka wachukue hatua
za haraka kuzuia maambukizi ya homa hiyo inayosababishwa na mbu
anayejulikana kitaalamu kama aedes egyptiae.
Hadi sasa wagonjwa zaidi ya 100 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika
wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke na baadhi wakiripotiwa kupoteza
maisha.
Daktari kiongozi wa hospitali hiyo ambaye pia ni mtaalamu wa ugonjwa
huo, Dk Mrisho Rupinda alisema kuwa kuna taarifa za wagonjwa wa dengue
walioripotiwa katika maeneo yote ya Dar es Salaam.
“Katika kipindi cha wiki moja iliyopita tayari madaktari wawili
kwenye hospitali hii wamebainika kuugua ugonjwa huo, tunahisi walipata
maambukizi kwenye maeneo ya humuhumu ndani hospitali,” alisema Dk
Rupinda.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
إرسال تعليق