Jumamosi iliyopita furaha iliwajaa mashabiki wengi wa Fid Q
akiwemo Mwana FA ambaye alimsindikiza Fareed Kubanda jukwaani kupokea
tuzo yake ya pili, na wakiwa jukwaani Mwana FA alizungumza kwa niaba
yake na kutoa ahadi kuwa kesho yake wangeingia studio kurekodi ngoma.

Hadi sasa Binamu pamoja na Fid Q hawajafanikiwa kuingia studio kama
walivyahidi na sababu zilizotolewa na FA ni kuwa wameamua kuipa muda
single mpya ‘Mfalme’, ambayo imeonekana kuwa gumzo toka alivyoi-perform
Jumamosi kwenye tuzo za Kili na kuitambulisha rasmi Jumatatu wiki hii.
“Bado hatujakaa sawa na Fid kauli yake anasema kwamba hii ‘Mfalme’
ina muda sana hebu tuchukue muda wetu wa kutosha kurekodi ngoma nyingine
kali, kwasababu hii Mfalme iko sana kwenye airwaves”. Alisema Mwana FA
kupitia Kwetu Flevah ya Magic Fm Jumatano wiki hii.
إرسال تعليق