Homa ya
uchaguzi mkuu wa Simba inazidi kupanda, baada ya Evans Aveva na Micheal
Wambura kuchukua fomu za kugombea urais wa klabu ya Simba SC, leo
wanachama maarufu wa klabu hiyo Godfrey Nyange Kaburu na Joseph
Itang’are maarufu kama Mzee Kinesi nao wamechukua fomu za kugombea
umakamu wa rais wa klabu hiyo.
Kaburu na
Mzee Kinesi wote waliwahi kushika nafasi za juu kwenye uongozi uliopita
wa Simba, lakini sasa wanaenda kwenye uchaguzi ujao wa Simba kuamua
nani atakuwa makamu wa kwanza kabisa wa klabu hiyo.
Risiti ya malipo ya fomu za kugombea umakamu za Kaburu
Post a Comment