MKONGWE wa filamu za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
ameibuka na kusema kuwa katika tasnia ya filamu hawezi kutokea msanii wa
kufanana na aliyekuwa msanii na muongozaji wa filamu, Adam Kuambiana.
Marehemu Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
Akistorisha na gazeti hili, Cathy alisema yeye na Kuambiana walikuwa
wakiishi maisha ya kutaniana, kila walipokuwa wakizungumza alikuwa
akimtania mambo mengi na siku moja kabla ya kifo chake alizungumza naye
kwenye simu kwa muda mrefu tofauti na siku nyingine huku akimtania sana.
“Nahisi kama Kuambiana alikuwa anajua anakufa maana siku moja kabla
ya kifo chake tuliongea kwa muda mrefu sana kwenye simu ukweli naumia
sana najiuliza kwa nini niliongea naye hivyo ila ndiyo hivyo tena Mungu
amempenda zaidi na ninaamini kwamba hakuna msanii anayeweza kufanana na
Kuambiana kwa ucheshi na utendaji kazi wake,” alisema Cathy.
Post a Comment