Kiwanda
hicho, Dangote Cement Obajana Plant, kinamilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa
Afrika, Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda cha saruji kikubwa kuliko
vyote Afrika Mashariki na Kati katika Kijiji cha Hiari Kata ya Namayanga,
mkoani Mtwara.
Rais
Kikwete katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini Nigeria,
Ijumaa iliyopita, aliamua kutembelea kiwanda hicho katika eneo la Obajana,
Jimbo la Kogi, kilometa 400 Kaskazini Mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara
wa Lagos.
Alipokewa
kwenye uwanja wa ndege wa kiwanda hicho na
Dangote mwenyewe, ambaye pamoja na mambo mengine alimuelezea manufaa
wanayopata wananchi wanaokizunguka.
Alimuelezea
Rais Kikwete kwamba kampuni yake inashiriki kwa karibu shughuli za jamii
zinazozunguka kiwanda hicho.
Miongoni
mwa shughuli hizo kwa mujibu wa Dangote, ni pamoja na kutoa huduma za elimu kwa
watoto na vijana wa wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Katika
kuboresha huduma hizo za elimu, Kampuni ya Saruji ya Dangote inajenga taasisi
kubwa ya elimu ya Dangote Academy, ambayo itatoa elimu na mafunzo ya ufundi kwa
ajili ya kuandaa wafanyakazi wa kiwanda hicho na watoto wa jamii inayozunguka
kiwanda hicho.
Pia
wananchi hao na familia zao, wananufaika na huduma za maji na umeme, na tangu
kiwanda kianzishwe mabenki 13
yalianzisha matawi yake katika eneo la kiwanda.
“Mheshimiwa
Rais, mbali na nyumba za wafanyakazi, tunawajengea hata nyumba za kuishi
wananchi wanaozunguka eneo hili ambao wanatuunga mkono sana,” alisema Dangote
Rais
Kikwete ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya Uchumi
Duniani-Afrika (WEFA) mwaka huu, mbali na kujionea na kupata taarifa za manufaa
kwa wananchi waliozunguka uwekezaji huo, pia alipata taarifa na kujionea
uwekezaji wa kiwanda hicho kikubwa cha saruji duniani.
Mbali
na uwanja wa ndege wa kiwanda ambako Rais alipokewa na Dangote mwenyewe,
pia alitembelea machimbo ya kiwanda
hicho ambayo yako kilometa tisa kutoka kiwandani, ambako malighafi ya kiwanda
hicho husafirishwa kwa madaraja na mikada maalumu hadi kiwandani.
Dangote
alimwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa kiwanda hicho cha Obajana, kinazalisha
tani za kimetriki milioni 10.25 kwa mwaka na kukifanya kuwa kiwanda kikubwa
zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja.
Pamoja
na kufikia hadhi hiyo ya dunia, Dangote alimweleza Rais Kikwete kwamba bado
upanuzi wa kiwanda hicho unaendelea na ukimalizika, uwezo wake wa uzalishaji
utaongezeka na kufikia tani za kimetriki milioni 13 kwa mwaka ifikapo mwakani
2015.
Upanuzi
huo kwa mujibu wa Dangote ukimalizika, utakuwa umegharimu dola za Marekani bilioni
2.5, na biashara yake itaongezeka kuzidi ya sasa ambayo ina thamani ya dola za
Marekani bilioni mbili kwa mwaka.
Kiwanda
hicho kilianza kujengwa 2003 na kukamilishwa 2006 ambapo kilizinduliwa na Rais
Olusegun Obasanjo Mei 12, 2007, wiki
mbili kabla ya kustaafu urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja
na kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi Nigeria.
“Mheshimiwa
Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za kiwanda hiki na
viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria, unahitaji kukumbuka
kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria nzima ilikuwa na uwezo za
kuwazalisha tani za kimetriki za saruji milioni 1.5 tu.
“Sasa
tunataka kufikia hatua ya kuhakikisha kuwa eneo la Afrika Magharibi na hata
bara letu la Afrika, linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya bara letu. Na
tutafikia huko,” alisema.
Dangote
alisema ili kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa kiwanda hicho uliamua
kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho kwa kujenga, miongoni mwa hatua
nyingine, bomba ya kilomita 92 la kusafirisha gesi kutoka Ajaokuta hadi kwenye
kiwanda hicho.
Alipoulizwa
na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa Gridi ya Taifa,
Dangote alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na
tunadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua zinatuhakikishia
umeme wakati wote na kwa kiwango ambacho tunakihitaji.
“Tunatumia
gesi ama dizeli yetu wenyewe. Na wala siyo umeme tu, hata miundombinu ya eneo
hili ikiwemo daraja hili kubwa
linalonganisha eneo la machimbo na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais,”
alisema Dangote.
Mbali
na kujenga miundombinu ya umeme wake, Dangote alisema kiwanda hicho pia
kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya maji kusaidia uzalishaji wa
saruji bila kutegemea huduma ya maji ya Serikali.
Bwawa
hilo, ndilo linalotoa huduma ya maji kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
Ili
kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa zaidi,
Dangote ameagiza malori 6,000 kutoka China kusaidia ujenzi na pia ameagiza
maelfu ya vibarua kutoka nchi hiyo hiyo ya China, kwenda kushiriki katika
ujenzi huo na kuumaliza kwa haraka.
Dangote
alimwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya jitihada kubwa kuhakikisha
anakifungua kiwanda cha saruji cha Mtwara kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka
ujao.
Tayari
mwishoni mwa Mei mwaka jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliweka jiwe la msingi
la ujenzi wa kiwanda hicho mbele ya uongozi wa Mkoa, mawaziri na mabalozi
kutoka nchi za Urusi, Misri, Angola, Nigeria na Kenya.
Pinda alisema ujenzi wa kiwanda hicho ni mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwa sekta ya ujenzi inachangia katika kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Mahitaji ya saruji nchini kwa sasa ni tani milioni tatu na viwanda vinne vilivyopo nchini kwa sasa vinazalisha tani milioni 1.2 sawa na mifuko 70,000 kwa siku, kiasi ambacho ni kidogo sana,” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, alisema kiwanda hicho kitazalisha tani milioni tatu kwa mwaka sawa na mifuko 150,000 kwa siku na kutoa ajira za moja kwa moja 1,000 na ajira zisizo za moja kwa moja 9,000.
Waziri Mkuu alisema viwanda vilivyopo nchini vinakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kukosekana kwa umeme wa uhakika, malighafi ya mawe ya chokaa ambayo huhitajika kwa asilimia 80 kwenye uzalishaji, gesi ya kuyeyusha mawe hayo na kwamba gharama kubwa ya saruji inasababisha isinunulike.
Alisema kutokana na kugundulika kwa gesi asilia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara, itakuwa maalum kwa ajili ya viwanda vya saruji, kwa kuwa malighafi muhimu ya gesi na mawe inapatikana kwa uhakika hasa mkoani humo katika Kijiji cha Msijute.
Alisema iwapo saruji itapatikana italeta mabadiliko makubwa kwani wananchi wa mkoa huo watainunua kwa bei rahisi na kujenga nyumba za kisasa.
Pinda alisema kampuni zingine 51 zimewasilisha maombi ya kuwekeza mkoani humo katika Kituo cha Uwekezaji (TIC).
Kampuni hizo na idadi ya miradi kwenye mabano ni mitambo ya luninga na redio (3), kilimo
(2), usindikaji korosho (7), majengo ya kampuni na ofisi (2), majisafi (2),
bidhaa zitokanazo na saruji (3), mbolea (1), mikate (1), matangi ya mafuta (2),
kiwanda cha ujenzi wa maboti (1), mbao (1), utalii (14), uchimbaji na
watafutajia wa mafuta (1), usafirishaji (8) na plastiki (1).Pinda alisema ujenzi wa kiwanda hicho ni mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwa sekta ya ujenzi inachangia katika kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Mahitaji ya saruji nchini kwa sasa ni tani milioni tatu na viwanda vinne vilivyopo nchini kwa sasa vinazalisha tani milioni 1.2 sawa na mifuko 70,000 kwa siku, kiasi ambacho ni kidogo sana,” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, alisema kiwanda hicho kitazalisha tani milioni tatu kwa mwaka sawa na mifuko 150,000 kwa siku na kutoa ajira za moja kwa moja 1,000 na ajira zisizo za moja kwa moja 9,000.
Waziri Mkuu alisema viwanda vilivyopo nchini vinakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kukosekana kwa umeme wa uhakika, malighafi ya mawe ya chokaa ambayo huhitajika kwa asilimia 80 kwenye uzalishaji, gesi ya kuyeyusha mawe hayo na kwamba gharama kubwa ya saruji inasababisha isinunulike.
Alisema kutokana na kugundulika kwa gesi asilia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara, itakuwa maalum kwa ajili ya viwanda vya saruji, kwa kuwa malighafi muhimu ya gesi na mawe inapatikana kwa uhakika hasa mkoani humo katika Kijiji cha Msijute.
Alisema iwapo saruji itapatikana italeta mabadiliko makubwa kwani wananchi wa mkoa huo watainunua kwa bei rahisi na kujenga nyumba za kisasa.
Pinda alisema kampuni zingine 51 zimewasilisha maombi ya kuwekeza mkoani humo katika Kituo cha Uwekezaji (TIC).
Post a Comment