Ule msumeno wa kuzifungia video za wasanii kutooneshwa katika
vituo vya TV umelikumba kundi la Sauti Sol kutoka Kenya, ambao wiki hii
wameachia video iliyoonekana kupokelewa vizuri na mashabiki wengi, toka
ilipowekwa youtube April 29 hadi leo tayari imetazamwa mara 143,892.
Akiongea wakati wa tukio la tuzo za Mdundo jana jijini Nirobi, member
wa kundi hilo Bien Aime alisema kuwa video ya ‘Nishike’ imefungiwa
kuoneshwa na vituo vya TV vya Kenya na sababu walizopewa ni kuwa
inachochea ngono.
Hiyo si video ya kwanza kufungiwa Kenya, video nyingine iliyowahi kufungiwa Kenya ni pamoja na ‘You guy’ ya P-Unit.
Source: Ghafla
إرسال تعليق