Ligi
kuu ya Hispania (LFP) imeipa adhabu klabu ya Villareal kutokana na kosa
la shabiki wao kumfanyia vitendo vya kibaguzi mchezaji wa FC Barcelona
mbrazil Dani Alves.
LFP imeiadhibu Villareal kwa faini ya
12,000 euros ($16,000) baada ya mmoja wa mashabiki wao kumtupia ndizi
beki huyo wa Barcelona kwenye mchezo baina ya timu hizo uliopigwa kwenye
dimba la El Madrigal.
Tukio hilo lilotokea kwenye mchezo ulioisha
kwa sare ya 1-1 lilitengeneza vichwa vya habari ulimwenguni kote,
kupelekea watu wengi kupiga picha wakiwa wanakula ndizi kuonyesha
kupingana na matukio ya ubaguzi wa rangi.
Shabiki huyo wa Villarreal ambaye tayari kafungiwa maisha na klabu hiyo kwenda uwanjani kuangalia mpira.
إرسال تعليق