
Ni mwakilishi wa Wadi ya Kiogoro Kaunti ya kisii huko Kenya na sasa
amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kudai kwamba Rais Uhuru Kenyatta
anavuta Bangi ambapo ishu ilianzia pale alipokaririwa Kanisani
akihutubia na kusema ‘walio karibu na Rais Uhuru Kenyatta sharti
wamshauri aache kuvuta Bangi’’
Kiongozi wa mashtaka ameiambia mahakama ya kisii kwamba mwakilishi
huyo wa wadi alitoa matamshi hayo katika kijiji cha karera na sheria
inayo mshtaki mtuhumiwa inasema ni hatia kwa yeyote kutoa matamshi kama
hayo kuhusu mtumishi wa umma .
Samuel ambae ni baba ya watoto watano anataaluma ya Teknolojia ya
maabara kutoka chuo kikuu cha Teknolojia Mombasa na amewahi kuhudumu
katika ofisi za hazina ya ustawishaji eneo Bunge kabla ya kuingia kwenye
siasa mwaka wa 2007 na baadae kuchaguliwa mwaka uliopita kuwa
mwakilishi wa Wadi.

Mshtakiwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000 pesa za Kenya na Kesi hiyo itatajwa May 14 na kusikilizwa June 3 2014.
Post a Comment