Kim & Kanye, KIMYE VOGUE Magazine COVER yauza kuzidi Beyonce na Michelle Obama

Capture
Wakati picha za ukurasa wa mbele wa Jarida maarufu la “Vogue” zilipotolewa rasmi mtandaoni huku wahusika wakuu wakiwa ni ‘Kanye West’ na ‘Kim Kardashian’, mastar wengi walijitokeza na kuamua kutonunua jarida hilo mara tu litapotoka rasmi na sababu kubwa ya wao kupinga uamuzi wa Vogue kuwaweka wapenzi hao katika ukurasa wa mbele wa jarida hilo.
Zikiwa zimepita siku chache tu toka jarida hilo limeachiwa, jarida hilo limeweka historia kwa kutafutwa zaidi na wanunuzi. Inadaiwa kua mpaka sasa kopi zaidi ya 500,000 jarida hilo zimeshauzwa ndani ya mda mfupi tu na hii imewashangaza watu wengi kwani Kim na Kanye wameweza kuuza kopi nyingi zaidi na kuwashinda ‘Beyonce’ mwaka 2013 ambapo ziliuzwa kopi  350,000 na hata mke First Lady Michelle Obama ambae ziliuzwa kopi 300,000 tu.
Report zinasema kuwa watengenezaji wa jarida la Vogue waliamua kuchapisha majarida zaidi baada ya stock  ya mwanzo kuisha mapema na ni kitu ambacho hawakukitarajia.

Post a Comment

Previous Post Next Post