Zikiwa zimepita siku chache tu toka jarida hilo limeachiwa, jarida hilo limeweka historia kwa kutafutwa zaidi na wanunuzi. Inadaiwa kua mpaka sasa kopi zaidi ya 500,000 jarida hilo zimeshauzwa ndani ya mda mfupi tu na hii imewashangaza watu wengi kwani Kim na Kanye wameweza kuuza kopi nyingi zaidi na kuwashinda ‘Beyonce’ mwaka 2013 ambapo ziliuzwa kopi 350,000 na hata mke First Lady Michelle Obama ambae ziliuzwa kopi 300,000 tu.
Report zinasema kuwa watengenezaji wa jarida la Vogue waliamua kuchapisha majarida zaidi baada ya stock ya mwanzo kuisha mapema na ni kitu ambacho hawakukitarajia.
إرسال تعليق