Umemiss kusikia Nay wa Mitego akitema maelezo juu ya midundo
ya hip hop? Kama ndiyo The bad The True Boy is right here na anatoa
kitu kipya cha hip hop ambacho bila shaka kitaichafua hewa kama kawaida
yake.
Nay wa Mitego aliyejipatia umaarufu zaidi kwa kufanya nyimbo zenye
mashairi tata, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa hivi karibuni ataachia
ngoma mpya ya Hip Hop ambayo itakuwa tofauti na ile atakayoifanyia video
Afrika Kusini.
“I hope ngoma itakayofuata ni ya hip hop…muda sio mrefu sana mimi
ntakuwa naachia ngoma. Yaani muda sio mrefu sana…sidhani kama zitaisha
wiki mbili au tatu. Wiki mbili haziwezi kuisha nitakuwa na- release
ngoma yangu ya hip hop, any time. Labda hii niseme ni exclusive kabisa.”
Nay wa Mitego ameiambia tovuti ya Times Fm..
Ameeleza kuwa yeye anaipenda sana hip hop kwa kuwa ndiyo
iliyomtambulisha na ikafanya apendwe na watu kabla ya huu muziki
aliufanya kipindi cha hivi karibuni.
Rapper huyo amerusha tufe kwa wale wanaosema kuwa yeye sio mwana hip
hop na kueleza kuwa inawezekana hivi sasa yeye ndiye msanii pekee wa
kweli anaefanya hip hop ukiwaondoa wakongwe kama Profesa Jay.
“Wapo wasanii wanafiki ambao wanasema wao wanafanya hip hop mimi sio
mwana hip hop shauri yao watakufa njaa. Mimi ni mmoja kati ya wana hip
hop wanaofanya hip hop ya kweli…peke yangu. Zamani naweza kusema
walikuwepo akina Profesa Jay akina nani.” Amefunguka.
“For this time nimebaki mwenyewe coz hip hop ni ukweli. Nani anaongea
ukweli? Mimi ninaongea ukweli. Mimi ni mwanahip hop sema mimi ni
mfanyabiashara. Wanabadilika akina Snoop Doggy wanahip hop wakongwe
wanaheshima kubwa sana duniani na bado wanaendelea kuitwa wanahip hop.
Nini Bongo! Bongo unajua kumekuwa na unafiki mwingi, kuna watu wanaona
kama ‘sisi ndio’ wakati ‘wao sio na sisi ndio’.”
Mkali huyo wa Itafahamika amesisitiza kuwa wimbo huo utaamsha kama ilivyokuwa nyimbo zake nyingine.
“Ngoma ya hip hop inafuata muda sio mrefu, watu wanajua ni kitu gani
huwa nafanya nikifanya ngoma ya hip hop so wajiandae nafikiri homa ya
jiji inakuja.”
Amesema ngoma hiyo imetayarishwa na ‘Mr. T Touch’. Kuhusu jina la
wimbo, “Sijajua itaitwaje lakini ndani ya siku mbili tatu hizi tutakuwa
tumeshajua itaitwaje…sijui itwaitwa ‘Utakula Jeuri Yako’..sijui nini
hata sielewi (anacheka).
Endelea kusikiliza 100.5 Times Fm na kutembelea tovuti ya Times Fm uwe wa kwanza kuisikiliza ngoma hiyo.
Msikilize hapa:
إرسال تعليق