Wakala
wake anasema kama club hiyo isipompa heshima Yaya Toure anaweza
kuondoka wakati wowote kwa sababu hakuna mchezaji yeyote au mtu yeyote
anaependa kufanya kazi kwenye ofisi ambayo haimuheshimu ndio maana
anaionya Manchester City imuombe msamaha.
May 13 2014 Yaya alitimiza umri wa miaka 31 hivyo alitegemea club
yake ingempa heshima au kuipa nafasi siku yake ya kuzaliwa lakini badala
yake ikachukuliwa poa tu, kitendo kilichomkasirisha Yaya na kuwamaind
viongozi wa club hiyo.
Pamoja na kwamba hajawakasirikia wachezaji wenzake, unaambiwa
walipokua kwenye ndege kuelekea Abu Dhabi kusherehekea ubingwa wao
inadaiwa wachezaji wenzake walipendekeza muhudumu wa ndege ndio
ampelekee Yaya keki ya birthday.

Wakala wa Yaya anasema ‘Yaya amefanya mengi kwa ajili ya Manchester
City, inasikitisha kwenye siku kama hii kuona hakuna kupewa mkono wa
pongezi kutoka watu wanaofanya kazi sehemu moja, amekasirika kwa kweli…
hii sio kawaida, hatutaki pesa wala zawadi bali attention, atleast
tambua umuhimu wa hiyo siku kwa mchezaji mkubwa ndani ya club… hauwezi
kuupata uhusiano mzuri kwa pesa au kuununua, inatakiwa wafanye hii
kutoka moyoni’
Kwa kuongezea Yaya Toure aliandika kwenye page yake ya twitter kwamba
maneno yote yaliyosemwa na Wakala wake ni ya kweli na kwamba yeye
mwenyewe atafanya interview baada ya kombe la dunia kuzungumza kila
kitu’

Kwenye sentensi nyingine Wakala huyu wa Yaya Toure alipoulizwa kama
Yaya ataendelea kubaki Manchester City baada ya kombe la dunia
kumalizika, amejibu ‘sijui…. Yaya mwenyewe ataongea na Man City kisha
tutafanya maamuzi baadae, ni club nyingi zinamtaka hivyo hakutakua na
kazi ngumu kupata kazi sehemu mpya’
إرسال تعليق