Hili NdioTamko walilotoa Beyonce, Solange na Jay Z kwa pamoja kuhusu tukio la Solange kumpiga Jigga ndani ya lifti

Beyonce, mume wake Jay Z pamoja na dada yake Solange Knowles wamevunja ukimya kwa kutoa tamko la pamoja kuelezea tukio la ugomvi wa kifamilia lililotokea May 5 ndani ya lift na video yake kuvuja.
beyonce-jay-z-solange-elevator-fight
“Kama matokeo ya kuvuja kwa video ya ‘elevator security’ kutokea Jumatatu, Mei 5, kumekuwa na vumi mwingi kuhusu chanzo cha tukio hilo la bahati mbaya” Walieleza katika tamko hilo kwa shirika la habari The Associated Press.
Waliendelea,
“lakini kitu cha muhimu ni kwamba familia yetu imelifanyia kazi swala hilo..Jay na Solange kila mmoja amewajibika kwa sehemu yake kwa kile kilichotokea. Wote wawili wameombana radhi kila mmoja na tumeendelea kuwa familia moja. Taarifa za Solange kulewa au kuonesha tabia isiyoeleweka jioni ile ni za uongo.”
Pamoja na kutozungumzia sababu za kilichotokea lakini walitisha kuwa wameyamaliza,
“Mwisho wa siku kila familia huwa na matatizo na sisi hatuna tofauti na familia zingine. Tunapendana na kubwa kuliko yote sisi ni familia. Tumeyaacha haya yamepita na matumaini yetu kila mtu mwingine yoyote atafanya hivyo pia.”
Video isiyokuwa na sauti iliyovuja Jumatatu na kuwekwa TMZ ilimuonesha dada yake Beyonce, Solange akimshambulia shemeji yake Jay Z ndani ya lift, na baadae kuwa tukio lililozungumziwa kila pande ya dunia kama habari kubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post