Beyonce, mume wake Jay Z pamoja na dada yake Solange Knowles
wamevunja ukimya kwa kutoa tamko la pamoja kuelezea tukio la ugomvi wa
kifamilia lililotokea May 5 ndani ya lift na video yake kuvuja.

“Kama matokeo ya kuvuja kwa video ya ‘elevator security’ kutokea
Jumatatu, Mei 5, kumekuwa na vumi mwingi kuhusu chanzo cha tukio hilo la
bahati mbaya” Walieleza katika tamko hilo kwa shirika la habari The
Associated Press.
Waliendelea,
“lakini kitu cha muhimu ni kwamba familia yetu imelifanyia kazi swala hilo..Jay na Solange kila mmoja amewajibika kwa sehemu yake kwa kile kilichotokea. Wote wawili wameombana radhi kila mmoja na tumeendelea kuwa familia moja. Taarifa za Solange kulewa au kuonesha tabia isiyoeleweka jioni ile ni za uongo.”

Pamoja na kutozungumzia sababu za kilichotokea lakini walitisha kuwa wameyamaliza,
“Mwisho wa siku kila familia huwa na matatizo na sisi hatuna tofauti
na familia zingine. Tunapendana na kubwa kuliko yote sisi ni familia.
Tumeyaacha haya yamepita na matumaini yetu kila mtu mwingine yoyote
atafanya hivyo pia.”
Video isiyokuwa na sauti iliyovuja Jumatatu na kuwekwa TMZ
ilimuonesha dada yake Beyonce, Solange akimshambulia shemeji yake Jay Z
ndani ya lift, na baadae kuwa tukio lililozungumziwa kila pande ya dunia
kama habari kubwa.
إرسال تعليق