Jaguar amethibitisha kuwa hana shida na posho na hela ndogo
ndogo za serikali ya Kenya kwa kuitosa ofa aliyopewa na gavana wa
Nairobi yakuwa member wa bodi ya vijana.
Kupitia barua aliyomwandikia gavana huyo, Jaguar ametaja sababu nne
za kukataa ofa hiyo ikiwa ni pamoja na kwamba ‘tangu serikali ichukue
madaraka mwaka uliopita sijaona ilichokifanya kwa vijana’, hakutaarifiwa
na serikali kabla ya jina lake kuandikwa kwenye gazeti na pia kutokuwa
na muda wa kuhudhuria vikao vya bodi hiyo.


إرسال تعليق