
Wakichukua maneno aliyoandika kwenye Twitter, si rahisi kuyaamini maana msanii huyu ameshajiingiza katika matatizo mengi ya kuvunja sheria. Beiber alishitakiwa na kesi yakuendesha gari lake na leseni iliyopita mda wake kwenye mji wa Miami, vile vile kipindi cha nyuma pia alishitakiwa na kesi ya kumvamia jirani yake na na kugonga gari kwa nyuma.
Sasa kuna mwanamke mmoja aliyekuwapo usiku ule wa wizi,amewapigia TMZ Live nakuelezea alichokiona. “Bieber hakushika mfuko wala mkoba wake, Bieber hakumwongelesha jambo lolote bali yule mama alikuwa aking’ang’ania kuchukuwa picha na msanii huyo. Bieber alikataa ila ule mama aling’ang’ania mpaka Iliwabidi walinzi wake wamwondoe yule mama maana alikuwa mkaidi sana. Mtoto wake wa miaka 13 alibakia akilia huku akiwa ameshika simu yake mkononi ila Bieber hakujaribu kumwibia au kunyang’anya .
Post a Comment