
“Nikiolewa wakati huu ,nataka ndoa yangu idumu na kufanya ndoa yako idumu si kazi rahisi. Lazima ujitoe kila kitu kwa mume wako.Kwa jambo hilo lazima uvumilie majaribu yote utakayo kumbana nayo na ujifunze kusamehe.
Kulingana na yeye, kabla ya kuamua kufunga ndoa na mwanaume yeyote, atamuuliza kama yuko tayari kumsamehe kwa jambo lolote na jibu ni hapana, sio mwanamume wakumfaa.
“Kama unajua kumuangalia mtu machoni na kumwambia ndio, hivo ndo utakachofanya kwangu. Ukinidanganya kwa mara ya kwanza, nitakusamehe. Ukijibu ukweli na ukawa na uhakika mwenyewe, hapo utajua kama huyo mtu ndiye anaye kufaa”
Genevieve aliendelea kwa kusema kwamba kila mwanamke anataka kuolewa ila tatizo nikumpata mwanamume anayeendana naye, mimi mwenyewe nilipata fursa yakuolewa sema niligudua kuolewa sio tatizo ila nikufaana.
Mwanamke mmoja alisema nataka kuolewa ila niwe na mwanaume anaye nifaa. Mimi ni mwanamke nahitaji kuwa na furaha kwa sababu nimezoea mienendo flani ya maisha.
إرسال تعليق