Mfungwa
mmoja amefariki Marekani kwa mshtuko wa moyo baada ya kuchomwa sindano
yenye lethal (lethal injection) yenye Mchanganyiko wa dawa tofauti kwa
ajili ya kuua.
Clayton Lockett alitakiwa kuuliwa baada ya kesi ya mauaji katika
gereza la Oklahoma lakini kabla ya hapo alichomwa sindano hiyo na
kufariki baada ya dakika 13.
Wiki iliyopita Lockett na mfungwa mwingine walipangiwa kuuliwa
kupitia dawa hiyo ya lethal ambapo mahakama ilithibitisha dawa hiyo
inakidhi mahitaji ya katiba lakini baada ya madhara kutokea kwa Lockett,
mfungwa mwenzake walietakiwa kuuliwa pamoja ameongezewa siku 14 mbele.
Baada
ya Lockett kufariki Wamarekani wengi wametoa maoni yao na kusema hukumu
hiyo ya kifo kwa Lockett ni sawa kabisa kutokana na makosa
aliyoyafanya.
Lockett alifungwa baada ya kuua msichana mwenye umri wa miaka 19
aitwae Stephanie Neiman kwa kutumia bunduki aina ya shotgun kutokana na
msichana huyo na rafiki yake kumsumbua wakati akiiba katika nyumba ya
mtu vilevile mahakama iligundua Lockett alimzika msichana huyo na kisha
kumbaka rafiki yake aliebaki.
Baada ya kuchomwa sindano Mwili wa Lockett ulikuwa ukitetemeka kwa
muda wa si chini ya dakika 13 kabla ya kufa kwake ambapo kifo chake
kimetafsiriwa kama kifo cha uzembe ambapo kumefanya kusimamishwa kwa
mauji ya aina hiyo baada ya kuonekana sindao hiyo haifanyi kazi
inavyotakiwa.
Wasimamizi wa mauaji hayo walianza kufunga mapazia ya chumba hicho
baada ya kuona Lockett akizidi kuwewesuka ambapo mmoja wa mashahidi wa
kitendo hicho amesema aliweza kuhisi jinsi Lockett alivyokuwa akiumia na
haikua njia ya kawaida kwa kuua mtu hata kama ana kosa gani.
Dawa hizo zilimfanya Lockett aonekane akizungumza bila ya kukamilisha hata neno moja.
Post a Comment