Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
limefanikiwa kubaini mtuhumiwa kinara wa wizi wa mabenki, Ronald Mollel (37),
ambaye ni mume wa Meneja wa Benki ya Barclays tawi la Kinondoni, Alune Kasililika,
anayeshikiliwa na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova (pichani), alitoa madai hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio ya ujambazi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova (pichani), alitoa madai hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio ya ujambazi.
Alisema Mollel
ni makazi wa Kimara Bonyokwa na
taarifa za kuaminika zinadai amekuwa akipanga njama na kushiriki kikamilifu
matukio mbalimbali ya uhalifu na kupora mabenki.
Alidai mtuhumiwa huyo ana mtandao na watumishi muhimu
katika matawi ya benki kwa lengo la
kufanikisha uhalifu katika benki hizo.
‘’Jeshi la Polisi tumeamua kuweka picha ya mtuhumiwa huyo hadharani kwa kutumia dhana ya
ulinzi shirikishi, ili akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo
chochote cha Polisi,’’ alisema Kova.
Pia alisema wamekamata watu watatu kwa tuhuma za
ujambazi wakiwa na silaha mbili aina ya Shotgun na risasi 12, Rediocall na sare
za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Isihaka Salehe, Alex
Andrew na Odinga Swalehe ambao
walikamatwa maeneo ya Chamanzi katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke.
Pia alisema jeshi hilo, limefanikiwa kuufumua mtandao
unaojihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam, ikiwemo uvunjaji na kupora
nyumba za ibada.
Alisema operesheni hiyo ilianza April 29 mwaka huu,
walikamata majambazi sugu wawili nao wakawataja wenzao 13.
‘’Watuhumiwa waliokamatwa katika mtandao mzima ni
Shaban Mafuru (36), mkazi wa Magomeni, Abdallah Hussein (52) mkazi wa Tabata
Mawenzi, walikutwa kwenye gari namba T259ADB,
’’ alisema.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa
wawili wakiwa na meno 25 ya kiboko na mmoja akiwa na vipande nane vya meno ya
tembo.
Post a Comment