Menejimenti ya Mamlaka ya
Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), imejikuta katika wakati mgumu, baada ya
wafanyakazi waliogoma, kukataa kurudi kazini
huku Serikali ikitoa masharti ya kuisaidia.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Yasin Mleke alisema mgomo huo unatokana na madai ya mishahara kwa miezi hiyo, ambayo hawajalipwa mpaka sasa na uongozi wa Tazara.
Phiri aliwaambia wafanyakazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tazara, ameitisha kikao cha dharura cha Bodi, kitakachofanyika kesho kwa lengo la kujadili tatizo hilo la wafanyakazi, ili kulipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tazara, Ronald Phiri jana
jioni alikutana na wafanyakazi katika kikao cha dharura, baada ya wafanyakazi
hao kugoma kufanyakazi mwanzoni mwa wiki hii, ambapo aliwaomba kurudi kazini,
lakini waligoma mpaka pale watakapolipwa mishahara yao ya Februari hadi Mei.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), Yasin Mleke alisema mgomo huo unatokana na madai ya mishahara kwa miezi hiyo, ambayo hawajalipwa mpaka sasa na uongozi wa Tazara.
Phiri aliwaambia wafanyakazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tazara, ameitisha kikao cha dharura cha Bodi, kitakachofanyika kesho kwa lengo la kujadili tatizo hilo la wafanyakazi, ili kulipatia ufumbuzi.
"Ombi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi na
kutoka kwangu, wakati tukisubiri kikao cha Bodi, siku ya Ijumaa turudi kazini,
ili majadiliano yatakayofanyika yazae matunda mazuri kwetu…tatizo hili liko
kote hata kwa upande wa Zambia," alisema Phiri.
Wafanyakazi walipotakiwa kunyoosha mikono walio
tayari kurudi kazini, hakuna aliyenyoosha. Lakini, walipotakiwa kunyoosha mkono
ambao hawako tayari kurudi kazini mpaka pale kikao cha bodi, kitakapokaa na
kutatua tatizo lao, wote walinyoosha na kusema kuwa hawako tayari kurudi
kazini.
Alipotafutwa jana, Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka, alisema Bodi ya Wakurugenzi ya Tazara walitoa
agizo kupata ufafanuzi ni wapi mishahara ya watumishi 100 wa shirika hilo,
ambao ni hewa inapokwenda, na kutaka shirika hilo kutoa taarifa ya fedha
walizonazo mpaka sasa.
Aidha, Dk Mwinjaka alisema kuwa mwishoni mwaka
jana Bodi hiyo ilitoa agizo kwa Menejimenti kulipa mishahara ya wafanyakazi
Februari kwa upande wa Tanzania, jambo ambalo halikufanyika mpaka sasa.
Post a Comment