Msanii nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija
Shaban maarufu kama ‘Keisha’ amejifungua mtoto wa kiume siku ya
Jumatatu (Mei 5) katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni.
Keisha akiwa amelala na mtoto wake
Akizungumza na Bongo5 leo Keisha,amesema anashukuru Mungu amejifungua salama na mtoto anaendelea vizuri. “Nimejifungua mtoto mwingine wa kiume katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni. Namshukuru Mungu nimejifungua salama na mtoto anaendelea vizuri,” amesema.
Mtoto wa Keisha
Post a Comment