TIMU
ya Mbeya City imewaambia Simba kuwa watoe dola 200,000 (zaidi ya
shilingi milioni 320) ili imuachie mshambuliaji wake tegemeo, Saad
Kipanga, kwa ajili ya kukipiga Msimbazi.
Mshambuliaji huyo alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rhino Rangers ya Tabora.
Mshambuliaji huyo alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rhino Rangers ya Tabora.
Kipanga hivi karibuni aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa, yupo tayari
kutua kuichezea Simba kwa dau la shilingi milioni 30 na mshahara wa
milioni moja kwa mwezi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa
Mbeya City, Mussa Mapunda, alisema kuwa hawatamzuia mshambuliaji huyo
kwenda kuichezea Simba, kikubwa kanuni na sheria zifuatwe.
Mapunda alisema kuwa, dau hilo walilolitangaza limetokana na muda alioubakiza wa mwaka mmoja na nusu kati ya miwili aliyosaini katika mkataba wake.
Mapunda alisema kuwa, dau hilo walilolitangaza limetokana na muda alioubakiza wa mwaka mmoja na nusu kati ya miwili aliyosaini katika mkataba wake.
Alisema kila mchezaji katika timu yao ana dau lake la usajili na
uwezo wa mchezaji ndiyo wanaouangalia kama timu nyingine ikimhitaji
kwenda kuichezea.
“Hatuwezi kumzuia mchezaji yeyote katika timu yetu kwenda kuichezea
timu nyingine kutokana na kwamba soka ni ajira inayoendesha maisha yao.
“Na kama mchezaji yeyote akiondoka kwenye timu yetu kamwe hataacha
pengo lolote kutokana na kuwepo wachezaji wengi wenye uwezo na vipaji
vya kucheza soka,” alisema Mapunda.
Post a Comment