Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa
kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta
ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama
anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa
kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini
yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto
kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.
Njia za kula Kondo la Nyuma
- Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
- Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
- Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini
muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia
anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.
'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa
maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na
kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa
kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza
biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya
pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola
hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu
wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza
kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo
la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading,
anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya
kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na
nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi
kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona
haraka,'' alisema mama Charlie.
'Kondo la Nyuma ni nini?'
Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka
mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama
anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu
hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama
wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.
Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji
hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni
huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya
magharibi.
'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.
إرسال تعليق